Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 16, 2012

Watoto wawili wa familia moja wateketea kwa Moto...!

Watoto wawili wa familia moja wakazi wa kimotoroko Wilaya ya Simanjiro
Mkoani Manyara wamefariki dunia baada ya nyumba yao walimokuwemo
ndani kuungua na kuteketea kwa moto kabisa.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro ,Akili
Mpwapwa wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani manyara.

Aidha kamanda Mpwapwa amesema kuwa tukio hilo lilitokea hivi karibuni
majira ya saa 10:00 jioni huko kimotoroko.

Amewataja watoto hao kuwa ni Luman Lck(5) na mdogo wake wenye umri
wa miezi minane(8) Leman lack ambao waliungua ndani ya nyumba yao na
kufariki dunia papo hapo.

Amebainisha kuwa chanzo cha moto huo ni kwamba watoto hao waliachwa
nyumbani wakichochea moto uliokuwa ukichemsha maharagwe jikoni huku
wazazi wao wakiwa wameenda kuchunga mifugo.

Ameongeza kuwa katika harakati za kuchochea moto ndipo moto huo
uliposhika chupa iliyokuwa na lita moja ya mafuta ya petroli iliyokuwa
karibu na moto huona kupelekea kulipuka na kushika nyumba hali
iliyopelekea kuungua na kuteketea kabisa.

No comments:

Post a Comment