Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 22, 2012

BEKI KUTOKA MALI ATUA MSIMBAZI...!


UJIO wa beki kutoka Mali, Komalmbil Keita unahatarisha maisha ya kiungo wa Simba, Mussa Mudde wa Uganda, ambaye ni majeruhi.
Hivi karibuni, Simba iliwavuta wachezaji wa kigeni, Mghana Danniel Akuffo na beki wa Kenya, Pascal Ochieng na

kufanya iwe na idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni.
Kutokana na hali hiyo, Simba sasa inatakiwa kupunguza mchezaji mmoja wa kigeni iwapo Keita atafuzu majaribio Msimbazi.
Kanuni za Ligi Kuu Tanzania zinaruhusu timu kuwa na wachezaji watano tu wa kigeni.
Simba iliwatambulisha Ochieng na Akuffo hivi karibuni lakini wote wamerudi makwao ili kuweka mambo sawa kabla ya kurudi nchini kuungana na kikosi hicho.
Wachezaji wengine wa kimataifa wa Simba ni Mganda Emmanuel Okwi na Mzambia Felix Sunzu pamoja na Mudde.
Komalmbil, anayecheza nafasi ya beki wa kati na kiungo akifuzu majaribio ina maana atajumuishwa kikosini na bahati nzuri mwisho wa uhamisho wachezaji wa kimataifa ni Septemba 10, mwaka huu.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza Mudde, ambaye anatakiwa kukaa nje kwa miezi mitatu yuko hatarini kupigwa panga.
Mudde atajikuta yanamkumba yale yale ya Mganda Derrick Walulya, aliyeachwa na Simba mwaka jana baada ya kuumia na kutotakiwa kutocheza kwa miezi mitatu baada ya kumalizika kwa Kombe la Kagame mwaka jana.
Simba inasemekana wanataka kumpa muda ili Mudde apumzike na kuangalia uwezekano wa kumrudisha kikosini Januari mwakani jambo ambalo ni kama njia ya kumfukuza kijanja.

No comments:

Post a Comment