Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, August 20, 2012

Dogo Janja Akubali Kufanya Kazi na Madee...!

Mwanamuziki chipukizi wa HIP POP nchini anayetokea mkoani Arusha ambaye miezi michache alikuwa gumzo kubwa sana kwenye vyombo vya habari anayejulikana kwa jina la Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ amesema hana bifu na mkongwe katika tasnia hiyo, Hamad Ally ‘Madee’ na kudai kuwa yupo tayari kufanya naye kazi.
Wawili hao walikuwa na tofauti siku za hivi karibuni kutokana na Dogo Janja kujitoa kwenye familia ya Tip Top Connection na kukwaruzana na Madee, ambaye ndiye aliyemkaribisha kwenye familia hiyo awali.
“Namuheshimu sana, Madee ni kaka yangu na sina bifu naye licha ya matatizo yaliyotokea hivi karibuni, nipo tayari kuimba nyimbo moja ya kushirikiana pamoja na kupanda jukwaa moja,” alisema Dogo Janja. Pia aliongezea kwa kusema "zile zilikuwa ni hasira tu kutokana na mambo mengi ambayo nikuwa nakisingiziwa na mojawapo likiwa la mimi kukataa shule kitu ambacho sio kweli"

No comments:

Post a Comment