Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, August 20, 2012

Gari ya Ommy Dimpoz yazua gumzo mitaani...!

 
Gari la Ommy Dimpoz aina ya Rav 4. Picha kwa hisani ya Millardayo.

MKALI wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amezua gumzo mitaani anakopita kutokana na mafanikio ya haraka anayoyapata, ambapo hivi karibuni alinunua gari aina ya Rav4 New Model kwa shilingi milioni 27.
Dimpoz alikuza jina kupitia wimbo wa Nai Nai aliomshirikisha Alli Kiba, alinunua gari hilo kutoka Kisiwani Zanzibar amesema: “Nimenunua Rav4 New Model kwa shilingi milioni 27, nafuatilia masuala ya usajili kwa kuwa lina usajili wa Zanzibar,” alisema Ommy mara baada ya ‘mkoko’ huo kutua kwenye ardhi ya Tanzania Bara.
Staa huyo ambaye pia ana asili ya Mkoa wa Kigoma, wiki iliyopita pia alikuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kutengeneza video ya wimbo wake wa Baadaye, sehemu ya video hiyo ilionyeshwa ambapo inaaminika kuwa itakuwa miongoni mwa kazi kali zilizofanywa na Kampuni ya Visual Lab ambayo ilisafiriki kutoka Tanzania kwenda nchini humo kwa ajili ya video hiyo.

Chanzo: Lucy Mgina

No comments:

Post a Comment