Msanii  wa bongo fleva Abdull Sykes ‘Dully Sykes’ amefunguka kuwa yupo tayari  kurudi shule. Akizungumza wiki iliyopita katika kituo cha redio Dully  alisema yeye binafsi hafichi kwani ameishia kidato cha pili na  kiingereza anachoongea ni kwa ujanja wake pamoja na marafiki zake wa  karibu kumfundisha, vilevile amewaasa vijana na wasanii wenzake nao  kusoma kwani dunia ya leo bila kusoma huwezi kusonga mbele, alimalizia  na kusema kuwa yeye hatakama hatopata nafasi ya moja kwa moja basi  atamtafuta mwalimu amfundishe hata nyumbani.

No comments:
Post a Comment