Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, August 14, 2012

Hali ya Ulinzi yaimarishwa nyumbani kwa Dk. Ulimboka...!

Baada ya Mweyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk.Steven Ulimboka, kurejea nchini kutoka afrika Kusini alikokuwa anatibiwa, hali ya ulinzi imezidi kuimarishwa nyumbani kwa wazazi wake alipofikia.Hali hiyo ilitokana na watu mbalimbali kujitokeza kwa wingi nyumbani kwa wazazi wake jana kumjulia hali Dk. Ulimboka na kuzuiliwa kuingia ndani kumuona.

Hali ya nyumbani kwa wazazi wake ilikuwa imebadilika tofauti na hapo awali baada ya kufungwa kwa geti kubwa katika mlango mkubwa wa kuingia nyumbani.

Awali kulikuwepo na ukuta ambao haukuwa na geti, huku baadhi ya watu wakisema ni kwa ajili ya usalama.Nje ya nyumba hiyo kulikuwepo na vijana waliokuwa wakiwafuatilia watu wote waliokuwa wakifika.

Paparazzi walifika nyumbani Ubungi Kibangi na kukuta umati mkubwa wa watu wakiwa ndani na nje ya nyumba hiyo kumjulia hali Dk. Ulimboka.

Kufuatia hali hiyo, Paparazzi walijaribu kuzungumza na baadhi ya watu waliofika nyumbani hapo akiwemo mama mzazi wa Dk, Ulimboka ambapo hakuwa tayari kuzungumza.

Baada ya waandishi kujitambulisha, baba mzazi aliwaamuru kuondoka eneo hilo kwa maelezo kuwa wanaotakiwa kufika hapo nyumbani ni ndugu na si watu wengine.

Tangu kutekwa, kuteswa kwa kupewa kipigo kwa Dk. Ulimboka, wazazi wake wamekuwa na wasiwasi na watu mbalimbali waliokuwa wakijitokeza kufika nyumbani kwao kuwafariji kwa tukio lililomkuta kijana wao.

Dk. Ulimboka alitekwa, kuteswa na kupata kipigo Juni 26, mwaka huu na watu wasiojulikana na kutelekezwa katika msitu wa Mabwepande na kuokolewa na msamaria mwema kisha kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) kabla ya kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
 
 
Chanzo: kwetubongo

No comments:

Post a Comment