Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 16, 2012

HOTUBA YA WAZIRI KIVULI NA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI NDUGU KABWE ZUBERI ZITTO KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWAMWAKA WA FEDHA 2012/2013.

UTANGULIZI...!
 
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kanuni ya 99(7),toleo la mwaka 2007 na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni,napenda kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzanikuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mafungu ya Wizara yaFedha-Fungu 50 Wizara ya Fedha, Fungu 21 Hazina, Fungu 22 Denila Taifa na Fungu 23 Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali. Vile vileFungu 10 Tume ya Pamoja ya Fedha na Fungu 13 Kitengo chaUdhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi.

Mheshimiwa Spika, mafungu yote yaliyo chini ya Wizara ya Fedhayanaomba kuidhinishiwa na Bunge lako tukufu jumla ya shilingi Bilioni4,208 (trilioni 4.2) ili yaweze kutekeleza majukumu yake. Mafunguhaya maombi yake ya Fedha ni sawa na asilimia 28 ya Bajeti nzimaya Serikali ya mwaka wa Fedha 2012/13.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha ndiyo msimamizi mkuu waUchumi wa nchi ikitekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo,kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani na ya nje, kusimamiamatumizi ya Serikali, kusimamia utendaji wa Taasisi na Mashirika yaUmma, kusimamia manunuzi ya Serikali na Taasisi na Mashirika ya Umma, kusimamia Deni la Taifa na dhamana za Serikali, kutafutasuluhisho na kusimamia mfumo wa kodi wa Serikali ya Jamhuri yaMuungano na kupambana na Fedha haramu. Sambamba na hayoni kusimamia na kutekeleza mpango wa kupunguza umasikini nchinikupitia utekelezaji wa MKUKUTA II.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha na mafungu yote yaliyo chiniyake ndio moyo wa Serikali na hivyo ni lazima kuitazama Wizara hiikwa jicho kali na kutilia mashaka kila jambo ambalo inalifanya ilikuhakikisha kuwa moyo huu hausimami maana madhara yake nikwa taifa zima na watu wake. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungenikupitia Waziri Kivuli wa Fedha inatekeleza wajibu huu kwa Uzalendo,Uadilifu na kwa misingi ya Uwajibikaji. Tumetekeleza wajibu huu natunaendelea kuutekeleza bila kujali maneno na kuweka maslahi yaTaifa letu mbele ya kila kitu kingine. Maslahi ya Taifa ni zaidi yavyama vya siasa, mahala tunapotoka au dini tunazoamini. Maslahiya Taifa ni kwa ajili ya Watazania na hasa Watanzania milioni 30 (TheBottom 30M) ambao bado wanaishi katika ufukara mkubwa sanawakikosa huduma muhimu za jamii na wanaoishi vijijini ambapohakuna umeme, barabara hazipitiki na wanahangaika kutwakutafuta maji safi na salama. Maslahi ya Taifa sio faida yawachache wenye kuishi mijini au wanasiasa wanaotafuta ushawishikwa umma bila kujali matakwa ya Umma. Watanzania wanyongewa vijijini wanajua maslahi yao ni nini. Wanajua kina nani Wanapigania maslahi ya Wanyonge.
    1. MAPATO YA SERIKALI
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya mwenendo waUchumi ya mwezi Julai (Monthly Economic Review, July 2012)iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania, katika kipindi cha mwezi JuniSerikali iliweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni
998.0. Hata hivyomatumizi halisi yalikuwa kiasi cha shilingi bilioni1,911.8 haliiliyopelekea kuwepo kwa nakisi baada ya kuondoa msaada wamasharti wa masharti wa shilingi bilioni 400.2; nakisi hiyo ililipwa kwavyanzo vya ndani na nje.



Mheshimiwa Spika, katika makusanyo hayo ya mwezi Juni Mamlakaya Mapato Tanzania ilikuwa imejiwekea lengo la kukusanya kiasi chashilingi bilioni 242.4 kama kodi ya Mapato, lakini ilikusanya kiasi chashilingi bilioni 366.0 kiasi ambacho ni zaidi kwa asilimia 60.8 yamalengo yaliyokuwa yamewe kwa.
Kambi ya Upinzani inapenda kulikumbusha Bunge na Taifa kwambakatika Bajeti Mbadala iliyowasilishwa hapa Bungeni tulisemakwamba TRA wanao uwezo wa kukusanya mpaka shilingi trillionmoja kwa Mwezi iwapo tutadhibiti misamaha ya kodi, tutakusanyakodi stahili katika Sekta ya Madini na tutasimama kidete kuzuiaukwepaji kodi wa Makampuni ya Kimataifa.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inaitaka Mamlaka ya MapatoTanzania kuimarisha zaidi marekebisho yanayofanyika katika mfumowa kodi ili kufikia lengo tajwa la kufikia makusanyo ya zaidi yaasilimia 20 ya Pato la Taifa. Mabadiliko kadhaa tunayoyafanyakwenye Sheria ya Fedha itakayosomwa hapa Bungeni katikamkutano huu wa Bunge yana lengo hilo la kupanua wigo wa kodina hivyo kulifanya Taifa lijitegemee.

2.1 Mauzo ya Nje
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha kupitia Benki Kuu ya Tanzaniainapaswa kuhakikisha kuwa Akiba ya Fedha za Kigeni nchiniinakuwa imara muda wote. Biashara ya nje ndio inaingiza Fedha zakigeni nchini kwa hiyo ni eneo la kutazama kwa makini na kuchukuahatua mwafaka. Taarifa ya mwenendo wa uchumi kwa mwezi Julaiiliyotolewa na Benki kuu inaonyesha kuwa jumla ya mauzo yaTanzania nje yalikuwa dola za kimarekani 7,990.0 milioniukilinganisha na kiasi cha dola 7,050.7 milioni kwa kipindi kama hichokwa mwaka 2011 na hali hii ilisababishwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuongezeka kwa bei ya mauzo ya dhahabu .
Hatahivyo Manunuzi yetu kutoka nje yamefikia dola za Kimarekani 12,959milioni.
Mheshimiwa Spika, , taarifa hiyo inaonyesha kuwa mauzo yadhahabu Nje kwa mwaka 2011 yalikuwa kiasi cha dola 2,330.7 milioni sawa na aslimia 56.7% ya mauzo yote nje, wakati mauzo yanje kutokana na bidhaa zilizozalishwa viwandani yalikuwa na jumlaya dola 922.0 milioni sawa na asilimia 22.4% ya mauzo yote ya nje.Aidha mauzo ya mazao mbalimbali kama Pamba, Katani, Korosho,Chai, Kahawa na mengineyo yalikuwa na thamani ya dola 761.1 milioni kwa kipindi hicho cha mwaka 2012.

Mheshimiwa Spika, taarifa hiyo imeendelea kuonyesha kuwatuliagiza bidhaa kutoka nje zenye thamani ya dola za Kimarekanimilioni 12,958.7. Katika manunuzi hayo tuliyofanya mafuta pekeyake yalikuwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni 3,586.1 ambalo ni ongezeko la asilimia 60.08% ukilinganisha na kipindi kamahicho kwa mwaka 2011. 

Mheshimiwa Spika, takwimu hizi zinaonyesha kwamba fedha zote zakigeni zilizotokana na mauzo ya dhahabu, bidhaa za viwandani naKorosho zilitumika kuagiza mafuta pekee yake! Hali hii ni mbayasana kwa uchumi wa Taifa letu na juhudi zote za kuongeza mauzonje zinaliwa na uagizaji wa Mafuta ambao umepanda sana katika siku za hivi karibuni.

Kambi Rasmi ya Upinzani inatambua kuwa kuanzia mwaka janaSerikali imekuwa ikitekeleza mpango wa Umeme wa dharuraambao umepelekea matumizi makubwa ya Mafuta. Hata hivyoieleweke kuwa Mpango mzima wa Manunuzi ya Mafuta yakuendesha mitambo ya Umeme inaligharimu Taifa Fedha nyingisana. Takwimu zinaonyesha kuwa Serikali inapaswa kutumia zaidi yashilingi 42 bilioni kila Mwezi kuendesha mitambo ya dharura yaUmeme. Manunuzi yenyewe ya Mafuta yamejaa mazonge yaufisadi uliokithiri. Licha ya kutaka Spika aunde timu ya kuchunguzaufisadi katika manunuzi ya Mafuta na licha ya Kamati ya Bungekutaka Uchunguzi wa kibunge kufanyika katika manunuzi hayabado hakuna hatua inayochukuliwa.
Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Mamlaka ya Manunuzi ya Umma PPRA kufanya uchunguziwa kina kuhusu manunuzi ya mafuta kuzalisha Umeme ambayoyanachoma bilioni 42 za Serikali kila Mwezi. PPRA hapaswi kufumbiamacho manunuzi yanayotafuna shilingi 1.4 bilioni kila siku nayanayoongeza manunuzi ya nchi kutoka nje (imports) na hivyokupoteza fedha za kigeni hovyo.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha ambayo ndio wizara mama yaPPRA kupitia Fungu 50, na ndio Wizara yenye kusimamia uchumi wanchi kwa ujumla ituletee Bungeni Taarifa ya Uchunguziutakaofanywa na PPRA kuhusu manunuzi shilingi 1.4 bilioni kila sikuya mafuta kuendesha mitambo ya kuzalisha Umeme.
2.3 Deni la Taifa.
Mheshimiwa Spika, Fungu 22 linaombewa jumla ya shilingi bilioni2,735 ili kuweza kulipa madeni ikiwemo deni la nje la shilingi bilioni373 na trilioni 1.5 kama deni la ndani. Kwa mujibu wa taarifa yamwenendo wa uchumi ya mwezi Julai 2012, deni la nje la Taifa(external debt) mpaka mwisho wa mwezi Juni 2012 lilikuwa limefikiakiasi cha dola za Kimarekani milioni 10,354.6 kiasi ambacho niongezeko la zaidi ya dola milioni
385.9 kwa kipindi kama hichomwaka 2011. Aidha katika kipindi hicho deni la ndani lilikuwa kiasicha shilingi bilioni
4,174.2 . Kambi ya Upinzani Bungeni ina taarifakwamba takwimu hizi za Deni la Taifa hazihusishi dhamana ambazoSerikali imezitoa kwa Mashirika ya Umma na Kampuni binafsi.Dhamana lazima katika siku za usoni ziwe ni sehemu ya deni la Taifamaana tumeshuhudia sasa ambapo Kampuni nyingi binafsizimeshindwa kulipa mikopo iliyodhaminiwa na Serikali. Mfano nimalipo ya deni lenye thamani ya shilingi bilioni 60 la kukodishandege ya Airbus kwa Shirika la ATCL kutoka kampuni ya WallisTraders ya Lebanon na Deni lililochukuliwa na Kampuni ya KiwiraCoal and Power limited ambayo mbia wake alishindwa kuendeshamradi wa Makaa ya Mawe Kiwira licha ya kudhaminiwa na SerikaliMkopo kutoka kwenye taasisi za Fedha hapa nchini ambapo sasaSerikali imepanga kulipa shilingi bilioni 40 katika Bajeti ya mwakahuu.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani haina tatizo nauhimilivu wa Deni la Taifa (Debt sustainability) kwani tunajua kuwamataifa makubwa yanakopa sana na yana uwiano mkubwa waDeni kwa GDP kuliko sisi. Tatizo letu ni namna ambavyo fedha zamikopo zinatumika. Matumizi ya mikopo tunayochukua sio endelevumaana sehemu ya mikopo hiyo hutumika kwa matumizi ya kawaidabadala ya matumizi ya uzalishaji au kuongeza uwezo wetu wakuzalisha. 

Kambi Rasmi ya Upinzani inaendeleza wito wake wa kutaka Fungu22 la deni la Taifa lifanyiwe ukaguzi maalum (Special Audit) ili tuwezekujua mikopo hii tunayochukua kila wakati inatumika kufanyia nini?Miradi iliyotekelezwa kutokana na Madeni ambayo Waziri wa Fedhaaliitangaza wakati wa kufunga mjadala wa Bajeti kuu ya Serikaliifanyiwe ukaguzi kutambua ukweli na kuona thamani ya Fedha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaendelea kuhojikama tulivyohoji mwaka 2011/2012 kuhusu matumizi mabaya yafedha za umma. Katika fungu 21, kasma 229929, Serikali imetengaShilingi bilioni 26.4 kwa ajili ya kulipa fidia kwa mikataba mbalimbaliambayo Serikali imeingia. Hii inaonyesha kuwa Serikali inatumiafedha nyingi sana kwa ajili ya mikataba iliyoingiwa na Mashirika yaUmma na kuliletea hasara Taifa.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani pamoja na kutakamajibu kutoka kwa serikali, bado tunataka kuwe na usimamizi thabiti ili kulinda fedha za umma zinazotumika kwenye Mashirika ya Umma,ambapo kumekuwa na usimamizi mbovu sana na unaopelekeaTaifa kupoteza fedha nyingi sana kutokana na ubadhirifu katikaMashirika ya Umma. Hii ni kweli kwa Mashirika ambayo Serikaliinamiliki sehemu ya hisa.
2.5 MKOPO WA KUNUNUA RADA ILIYOGUBIKWA NA UFISADI
Mheshimiwa Spika, sehemu ya Malipo ya Deni la Taifa ni Mkopoambao Serikali ilichukua ili kununua Rada kutoka kampuni ya BAE yaUingereza. Suala hili la rada limejadiliwa sana nchini kwa upandemmoja tu wa ufisadi wa kupandisha bei ya Rada na hatimayekurejeshwa kwa iliyoitwa chenji ya Rada. Hiyo ilikuwa ni nusu tu yaukweli kuhusu suala la Rada kwani Serikali ilikopa kiasi cha dola zakimarekani 40 milioni kutoka Benki ya Barclays ya Uingereza kwa ajiliya kununulia Rada. Mkopo huo ulikuwa na Riba ya asilimia 4.9 juu yakiwango cha riba zinazotolewa na Benki ya Dunia au IMF.
Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kujua kama mkopo huuumeshalipwa wote na jumla tulilipa kiasi gani cha fedha.Ukilinganisha fedha iliyorejeshwa kama chenji ya Rada na Fedhaambayo Tanzania iliilipa Benki ya Barclays (Principal amount naInterest), je chenji ya Rada ilikuwa na thamani yoyote kifedha?Mjadala wa ununuzi wa Rada hauwezi kuisha kwa kufurahiakurejeshewa chenji tu. Mjadala huu bado mbichi kabisa kwanitunataka ukweli na ukweli mtupu uelezwe kwa umma na kuona Taifa lilipata hasara kiasi gani kwa ufisadi huu wa kimataifa na hatuastahiki za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wote walioingiza hasara kwaTaifa letu.
2.4 Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu
Mheshimiwa Spika, taifa letu limekuwa na sheria nyingi ambazoziliwahi kutungwa kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la fedha haramu,rushwa na uhalifu uliopangwa hapa nchini mwetu tangu tupateuhuru na hii inathibitishwa na uwepo wa sheria zaidi ya 15 kuwahikutungwa tangu uhuru (tazama kiambatanisho A ). Vile vile Bungeliliimarisha Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu mwaka 2011. Hatahivyo bado nchi yetu imegubikwa na fedha chafu na hasa wizikatika Mabenki hapa nchini. Wakati sheria ya Fedha haramuinayataka Mabenki kutunza kumbukumbu sahihi za wateja,kumekuwa na matukio (yaliyoripotiwa na yasiyoripotiwa) yaWafanyakazi wa mabenki hapa nchini kushirikiana na baadhi yawananchi kuiba fedha za wateja na hasa wateja ambaowamefariki dunia na ndugu na jamaa zao kutojua taarifa za kibenkiza marehemu hawa. Serikali inapaswa kufahamu kuwa wizi kwenyemabenki ni moja ya sifa mbaya sana ya mfumo wetu wa fedha nahivyo kusababisha Benki kuweka riba kubwa sana ili kufidia ‘risk’kama hizi za watu ‘kupiga’ amana za wateja kwenye mabenki. Kambi Rasmi ya upinzani inaitaka Wizara ya Fedha kupitia Kitengo cha Udhibiti wa Fedha haramu kudhibiti wizi kwenye Benki za hapanchini.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kupatamaelezo ya kina juu ya matatizo ya mtaji “ Capital under pressure” yanayoikabili benki ya NBC na hatua zilizochukuliwa na Serikali kamammoja wa wanahisa dhidi ya mwanahisa mwenye dhamana yakuisimamia Benki hiyo (ABSA) kwa kushindwa kuisimamia kwaumakini na hivyo kuiingiza katika matatizo hayo ya mtaji.Mheshimiwa Spika, hivi sasa wanahisa (ambapo Serikali ni mmojawao) wanapaswa kuongeza mtaji katika benki ya NBC ili kuinusuru,Benki ambayo ni moja ya Benki kubwa kabisa hapa nchini ambayokama ingekuwa na usimamizi mzuri ingepaswa kujiendeshayenyewe na kutoa gawio kwa wanahisa.

Mheshimiwa Spika, taarifa iliyotolewa na Benki Kuu ya Uswissi nakuchapishwa na magazeti mbalimbali ya hapa nchini mwezi June,2012 inanonyesha kuwa viongozi wa Serikali pamoja nawafanyabiashara wakubwa wametorosha fedha zao katikamabenki ya Uswissi kiasi cha shilingi bilioni 315.5. Habari zaidizinaeleza kwa mba mabilioni haya yanatokana na ‘deals’ zilizofanywa na watendaji wa Serikali na wafanyabiashara kadhaakwenye sekta za Nishati na Madini. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniimepata taarifa kuwa mmoja wa Viongozi wa juu kabisa wa Tanzania na baadhi ya Mawaziri wa Serikali za awamu zilizopita nimiongoni mwa wamiliki wa Fedha hizi. Sehemu kubwa ya Fedhazililipwa na Kampuni za utafutaji wa Mafuta na Gesi katika Pwani yaMkoa wa Mtwara zilizopewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006.Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa taarifa rasmi yahatua gani imechukua mara baada ya taarifa ile kutoka Benki yaTaifa ya Uswissi ilipotolewa.
Tunaitaka Serikali kuliambia Taifa hatuaitakazochukua kurejesha fedha hizi na nyingine zozote ambazozimefichwa ughaibuni. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni italazimikakuweka wazi taarifa na majina ya watu wenye umiliki wa fedhakatika Benki za nchini Uswissi iwapo Serikali haitatoa taarifa rasmikuhusu suala hili. 

Mheshimiwa Spika, Aidha, kuna taarifa nyingine zinaonyesha jinsiambavyo taifa linaibiwa kupitia kesi mbalimbali ambazo Serikaliimeshitaki au kushitakiwa kwenye Mahakama za Kimataifa. Mfanomzuri ni Kesi ya IPTL na Standard Chartered Bank ya Hong Kongambayo imechukua muda mrefu bila kuisha na kuliingizia taifahasara kubwa sana. Tunapenda kufahamu ni kwa nini mpango wakumaliza kesi hii nje ya Mahakama hautekelezwi na vile vile mpangowa kugeuza Mtambo wa kufua umeme wa IPTL kuwa wa Gesi kwanini hautekelezwi?
Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kupata majibu kuhusu mamboyafuatayo; Kwanza, fedha zilizoko kwenye Escrow Akaunti Benki Kuu za IPTL(Tegeta escrow) zimefikia kiasi gani mpaka sasa, na usalama wafedha hizo ukoje? Ikumbukwe kwamba kuna uamuzi wa Bungekwamba Fedha hizi zisitumike wala kutolewa mpaka maamuzikuhusu mtambo wa IPTL kufikiwa na hasa uamuzi wa kugeuzamtambo huu kutumia Gesi Asilia.Pili, Suala hili la kesi ya IPTL limechukua muda mrefu sana na sasa niwakati muafaka likamalizwa nje ya mahakama kwa Waziri waFedha kukutana na pande zote za mgogoro huu ili liweze kufikiamwisho.
2.6 Kampuni ya Oxford University Press Tanzania KufungiwaMheshimiwa Spika, mnamo tarehe 03 Julai 2012 Benki ya Duniailitangaza kuifungia kampuni ya uchapishaji ya Oxford UniversityPress Tanzania Ltd (OUPTL) kutokana na vitendo vya rushwaambavyo kampuni hiyo ilikiri kuhusika kwake kwenye miradimbalimbali ya elimu iliyokuwa inafadhiliwa na Benki hiyo katikaukanda wa Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Spika, kampuni hiyo ilikiri kuhusika katika kuwahongamaafisa mbalimbali wa Serikali katika mkataba wake wakusambaza vitabu na kampuni hiyo ilikubali kuilipa Benki ya Duniakiasi cha dola 500,000 kama sehemu ya makubaliano yakekutokana na kashfa hiyo.
Mheshimiwa Spika, mamlaka ya manunuzi ya umma ilitangazakuifungia kampuni hiyo hapa nchini kwa kipindi cha miaka saba,wakati ambao tayari tulishawapa zabuni ya kusambaza vitabuvilivyotokana na chenji ya rushwa ya Rada ambazo ziliamuliwakuwa zitaenda kununua vitabu.
Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuinyang ’anya kampunihii zabuni ya kuchapisha na kusambaza vitabu hivyo na badalayake kazi hiyo yapewe makampuni ya ndani ya nchi. Tabia yaSerikali kufanya kazi na Kampuni ambazo tayari zina dosari ama zakifisadi au kukiuka sheria na maagizo ya Serikali inatoa picha mbayakwenye uchumi. Hali kadhalika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kuwachukulia hatua maafisa wote wa Wizara waliohusika katika “rushwa ya Oxford”.
3.0 Mishahara hewa nchini
Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmiya Upinzani kuhusu makadirio ya mapato na matumizi katika Ofisi yaRais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa mwaka wa fedha2012/2013, tulitaja kiasi cha shilingi bilioni 9 1 ambazo zililipwa kamamishahara kwa watumishi hewa kama ilivyoripotiwa na magazeti ya The Daily News’ na ‘The Guardian ’ya Machi 23, 2011.


Mheshimiwa Spika, ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabuza Serikali ya tarehe 31 Machi, 2012 inaonesha kwamba kwa mwakawa fedha 2010/2011 jumla ya shilingi 142,715,827.992 zililipwa kamamishahara kwa wastaafu, watumishi walioacha au kufukuzwa kazina watumishi wengine ambao hawakustahili. Aidha, ripoti hiyoimeonesha kiasi cha shilingi 1,842,607,565.29 zilizolipwa kamamishahara hewa kwa mwaka wa fedha 2009/2010.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Fedha kwakamati ya kudumu ya Bunge ya fedha na uchumi ya tarehe 7Agosti, 2012 ni kwamba uhakiki wa watumishi uliofanyika mweziJanuari, 2012 kwenye Halimashauri 133 na kwenye taasisi na wakalaza Serikali 154 ulibaini majina 9,949 ya watumishi wasiostahili kuwemokwenye orodha ya mishahara. Idadi hii ya watumishi hewa nisawasawa na takribani idadi ya watumishi walioajiriwa katika sektanzima ya madini kwenye migodi ya dhahabu hapa nchini.Watumishi hewa wanaokaribia 10,000 ni wengi mno na inaonyeshadhahiri namna Serikali isivyo makini katika suala hili ambalolinasababisha upotevu mkubwa wa Fedha za Umma.
Mheshimiwa Spika, Waziri wa Fedha alikiri mbele ya Kamati yaFedha na Uchumi kwamba mwezi Februari Serikali ililipa shilingi bilioni5.1 kama mishahara hewa. Hii maana yake ni kwamba Serikali. hutumia zaidi ya shilingi bilioni 70 kila mwaka kwa watumishi hewawa Serikali.
Mheshimiwa Spika, tunataka fedha hizi wanazolipwa watumishihewa zitumike kuwalipa walimu na madaktari madai yao kwani ninyingi na zinatosha sana. Siku zote sababu za Serikali kutotimizamatakwa ya wafanyakazi kwenye sekta ya Afya na Elimu nikwamba Serikali haina Fedha. Lakini hapa tunashuhudia Shilingibilioni 70 kila mwaka zikiteketea kulipa watumishi hewa ambaohawapo, hawafanyi kazi na hivyo kufaidisha mtandao wa kifisadiambao kwa vyovyote vile unaanzia Wizara ya Fedha na Wizara yaUtumishi. Serikali inakosa vipi fedha za kulipa madai ya Walimu nainapata za kulipa watumishi hewa? Serikali inakosa vipi fedha zakulipa Madaktari na Manesi lakini inapata shilingi bilioni 70 kilamwaka kulipa watumishi hewa?
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka mradi huu wawatumishi hewa wenye mauzo (turnover) ya shilingi 70 bilioni kwamwaka uvunjwevunjwe ili kupata fedha za kulipa Walimu naMadaktari. Waziri wa Fedha asambaratishe mtandao huu mwovuambao sasa umeota mizizi kwenye Taasisi za Serikali. Vile vile Waziriagawe kwa Wabunge taarifa ya uhakiki wa wafanyakazi wa Serikalina pia hatua ambazo Serikali imechukua dhidi ya vinara wamtandao wa watumishi hewa Serikalini.
4.0 Benki Kuu ya Tanzania-(BOT)
Mheshimiwa Spika, taasisi hii ndiyo yenye dhamana ya kutayarishana kusimamia sera za fedha na utendaji mzima wa taasisi za fedhakwa ujumla. Katika kutekeleza hilo Benki Kuu ndicho chombokinachoweka miongozo kwa taasisi za fedha, taasisi za bima nataasisi za hifadhi za jamii ili kuhakikisha fedha za wanachama katikataasisi hizo zinalindwa.
Mheshimiwa Spika, taasisi za fedha zimegawanyika katika sehemukuu mbili, ambazo ni tasnia ya benki (Banking industry ) na tasniandogo ya fedha (Microfinance industry). Tasnia zote hizizinahudumia wateja tofauti kwa kulingana na wanachojishughulishanacho katika kuinua kipato cha familia inayomtegemea, mteja yukokwenye sekta binafsi au sekta rasmi ya ajira.
Mheshimiwa Spika, Benki Kuu katika kutimiza wajibu wake inailazimukutoa vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji wa mikopo ilikukabiliana na wakopaji ambao wanaweza kuwa na lengo lakuchukua fedha wakati hawana nia ya dhati ya kurejesha mikopoyao.


4.1 RIBA KATIKA TAASISI ZA FEDHA
Mheshimiwa Spika, tofauti kati ya viwango vya riba vinavyotozwakwenye mikopo na vile vinavyotolewa kwenye amana kama faidavimeendelea kuwa juu, licha ya kuongezeka kwa ushindani katikasekta ya kibenki. Hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na kukosekanakwa taarifa sahihi za wakopaji (credit reference data bank) na kutokuwepo kwa taasisi ya utoaji wa taarifa sahihi za waombajimikopo (Credit Rerefence Bureau) nchini. Aidha, gharama kubwaza kufanya biashara kutokana na miundombinu hafifu, nazozimechangia kuongeza viwango vya riba vinavyotozwa kwenyemikopo. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaomba taarifa yakuanzishwa kwa Credit Reference Bureaux kwa mujibu wa Sheria yaBenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.
4.2 Usimamizi Wa Tasnia Ndogo ya Fedha (Microfinance Industry-MFI)
Mheshimiwa Spika,tasnia hii ndiyo inayoshughulika moja kwa mojana kundi kubwa la Watanzania ambao hawako kwenye mfumorasmi wa ajira kwa kuwapa mikopo midogo midogo kwa shughulirasmi au zisizo rasmi, ili kuhakikisha kuwa kipato cha familiakinapanda na hivyo uchumi wa mwananchi mmoja mmoja unakua.
Mheshimiwa Spika, tasnia hii inalenga kuboresha maisha yawananchi wa vijijini na maeneo mbalimbali ya mijini. Tasnia hiiinalenga kuboresha maisha kwa wananchi mmoja mmoja aumakundi (Saccoss) na benki jamii (vicoba) ambazo zimekuwa nawanachama wengi wanaoendelea kujiunga ili kujikwamuakiuchumi.
Mheshimiwa Spika, kukosekana kwa mdhibiti anayeelewa jinsi tasniahii inavyofanya kazi zake na aina ya wateja inaowahudumia ni udhaifu mkubwa unaosababisha tasnia hii kushindwa kukua.Kukosekana kwa udhibiti wa sekta ndogo ya Fedha kunasababishawananchi masikini kuumia sana. Mfano tumeshuhudia namnaKampuni za kukopesha zinavyowafanya Walimu vijijini kuwa masikinizaidi kwa kuweka riba kubwa sana. Hata hivyo Serikali imekaa kimyabila kusaidia wanyonge hawa kwa kuchukua hatua madhubuti zakudhibiti na kusimamia sekta hii. Mfano mzuri wa Serikali kushindwakusaidia wanyonge ni pale ambapo wannachi wengi sana kujikuta wamepoteza fedha zao kupitia ‘schemes’ kama vile DECI ambapo wananchi walikusanya zaidi ya shilingi bilioni 16 ambazo mpaka sasahata riba yake hatujui inakwenda wapi? Kungekuwa na Mamlakaya kusimamia sekta ya fedha kwa ajili ya wanyonge tusingeshuhudiaunyonyaji huu.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuundaMamlaka ya Usimamizi wa sekta ndogo ya Fedha (TanzaniaMicrofinace Regulatory Authority) hapa nchini badala ya Benki Kuuya Tanzania ambayo ndiyo msimamizi wa tasnia ya benki. Lengo nikuhakikisha kuwa wananchi wa vijijini wanaopata mikopo kutokakwenye taasisi za Benki wanalindwa na dola. Mamlaka italinda Haki za wanyonge dhidi ya ‘loan sharks’ na Wajibu wa wanyonge wenye kuchukua mikopo.
Mheshimiwa Spika, kuundwa kwa chombo chenye mamlaka yakusimamia taasisi ndogo ya fedha ni lazima kutokana na ukweli kwamba kuna utofauti wa muundo baina ya mabenki na taasisindogondogo za fedha; inakuwa ni vigumu kudhibiti riba na utoajiwavigezo vya kifedha katika kuhudumia wananchi na kutoamikopo kwa wateja wa tasnia hizo mbili zilizo tofauti kimuundo.
Mheshimiwa Spika, kuwepo kwa chombo chenye mamlaka piaitasaidia kuwa na Credit Reference Bureau itakalokuwa na taarifaza wakopaji kutoka taasisi ndogondogo za fedha tofauti naitakayosimamia wadaiwa wa mabenki na taarifa hizi zitasaidiaudhibiti wa wateja wa taasisi hizi kuchukua zaidi ya mkopo mmojakwenye taasisi tofauti tofauti ambapo hali hii husababishwa naucheleweshaji wa mikopo inayotolewa na taasisi hizi pamoja nauhafifu wa mikopo katika kumsaidia mlengwa.

4.3 Mifuko ya Hifadhi za Jamii
Mheshimiwa Spika,Mifuko ya Hifadhi za Jamii ni mojawapo ya sektaambayo ina uwezo mkubwa wa kupunguza ukosefu wa ajira kwavijana wetu, kama uwekezaji unaofanywa kwa kutumia mifuko hiyoutasimamiwa vizuri.
Meshimiwa Spika, inaonesha kwamba mifuko hii imekuwa ikikusanyamichango ya wanachama na kulipa wastaafu wanachama waMifuko hii vizuri. Kutokana na maelekezo ya sheria mpya iliyoletamjadala baina ya wafanyakazi na serikali juu ya mabadiliko yasheria na utoaji wa mafao kwa wafanyakazi, pamoja na Bungekutaka mabadiliko ya sheria hiyo bado kuna haja ya kutazamanamna mifuko ifanyavyo kazi.

Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka serikali kuweka wazi utendaji waMifuko hii katika maeneo nyeti yafuatayo, kwanza Ukwasi wake (Liquidity of the Social Security funds), pili Uwekezaji (Investments) piaRisk Management reports. Taarifa katika maeneo haya hupelekwana mifuko kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika yaUmma na kutokana na utaratibu wa Kazi wa Kamati hii ya POAC nivigumu wananchi wote kuona taarifa hizi ambazo ni muhimu kuwawazi kwa umma. Taarifa kama hizi zitaliwezesha Bunge kuelewakiwango cha usalama wa Mifuko hii na uwezo ziada (excessfinancial capacity) kuendelea kutoa huduma zinazohitajika. Kamailivyo kwa Mabenki, tunashauri kuwa taarifa za robo mwaka zaMifuko ya Hifadhi ya Jamii ziwe zinatangazwa kwenye magazetiyanayosomwa zaidi nchini ili wananchi na hasa wanachama wamifuko waone namna mifuko yao inavyofanya kazi.
Mheshimiwa Spika, aidha, kwa kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani kwakipindi chote imekuwa ikitoa ushauri katika sekta hii, hatuna budikurudia ushauri tulioutoa mwaka jana kama ifuatavyo: “
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inapendekeza kwa Mifukoya PSPF na PPF kuangalia namna ya kuwekeza katika maeneoyanayochochea ukuaji wa uchumi na hivyo kuzalisha ajira na kupata wanachama zaidi. Maeneo kama uwekezaji kwenyeBandari na Reli yanapaswa kuangaliwa kwani kutokana na Jiografiaya nchi yetu ni maeneo yanayoweza kuzalisha faida kubwa sana.Tunaitaka Serikali ilieleze Bunge kuna mipango gani katika Mashirikahaya (PSPF na PPF) kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji katikamiundombinu na hasa Bandari.
Mheshimiwa Spika, Mifuko ya hifadhi ya jamii imewekeza katikamiradi ya ujenzi wa nyumba nafuu kwa ajili ya wanachama wao napia wanachi kwa ujumla. Tunasisitiza Miradi hii isiwe Dar es salaamna Mwanza tu bali ienee nchi nzima kama ambavyo mfuko wa PSPFumeanza.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani pia inashauri kwamba fao laElimu ambalo Mfuko wa PPF unatoa kwanza litolewe na Mifukomingine pia lakini pia lipanuliwe hadi kufikia elimu ya Chuo Kikuu.Fao hili la Elimu ambalo ni muhimu sana na twapongeza mfuko waPPF kwa kulianzisha ni fao ambalo litasaidia sana kuhakikisha kuwayatima ambao wazazi wao wanakuwa wamefariki wanapatauhakika wa kuendelea na masomo. Fao hili liwe fao la lazima kwamifuko yote nchini.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni bado inasisitizaushauri wake kuwa
Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii ihamishiweWizara ya Kazi na Ajira kama Wizara inayo husika na ‘social security’. Hoja hii inatiliwa nguvu na uhalisia kwamba Mdhibiti wa Mifuko (SSRA) yupo chini ya Wizara ya Kazi. Vile vile Wizara ya Fedha kamamlipaji mkuu wa Pensheni asiwe na Taasisi hata moja ya Pensheni chini yake ili kuweka ‘checks’.
Mheshimiwa Spika, Hali kadhalika hakuna sababu ya kuwa na utitiriwa mifuko mingi kama ilivyo sasa. Ipunguzwe na kubakia na mifukomiwili tu, mmoja wa wafanyakazi walio katika sekta binafsi na sektaisiyo rasmi na mwingine kwa wafanyakazi wa sekta ya umma .Tunarejea pendekezo letu kwamba mifuko ya NSSF na PPFiunganishwe kuwa mfuko mmoja kwa ajili ya sekta binafsi na sektaisiyo rasmi na mifuko ya PSPF, LAPF na GEPF iunganishwe kuwamfuko mmoja kwa ajili ya kushughulika na wafanyakazi wa Sekta yaUmma”.

Mheshimiwa Spika, mojawapo ya vipaumbele vya Kambi Rasmi yaUpinzani kwa mwaka 2012/2013 ni kupunguza misamaha ya kodi yakutozidi asilimia moja ya GDP, kutokana na Mapato mengi ya Serikalikupotea kwa sababu ya kutoa misamaha ya kodi kwa wadaumbalimbali wanaotakiwa kulipa kodi, na ikizingatiwa moja yamichango ya waziri akiwa mbunge tarehe 25/8/2011 alisema “kupunguza misamaha ya kodi ya kutozidi asilimia moja ya GDP”.Kambi Rasmi ya Upinzani inaamini waziri alikuwa na nia ya dhati nakukubaliana na Kambi Rasmi ya Upinzani uwezekano wa jambo hili.Hivyo basi, ili kuonesha kuwepo kwa dhamira ya kweli Kambi Rasmi ya Upinzani inataka waziri alijulishe bunge juu ya utekelezaji waazimio hili.
6.0 MSAJILI WA HAZINA NA BODI ZA MASHIRIKA YA UMMA.
Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa mnamo mwaka 2010 Sherianamba 2 (the written laws (miscellaneous amendments) No 2. ACT2010 ilipitishwa na katika eneo la kumi (part X) ilifanyia marekebishosheria ya mashirika ya umma (the public Corporations Act, CAP257). Sheria hii ilisainiwa na Rais mnamo tarehe 20 Mei 2010.
Mheshimiwa Spika, katika mabadiliko hayo ya sheria ibara ya 20 na21 ilibainisha bayana majukumu ya msajili wa hazina na ndipoiliweka majukumu yake ya kazi kuwa ni kusimamia mashirika yote yaumma. Aidha, mabadiliko hayo yalibainisha wazi kuwa msajili wahazina hatakuwa mjumbe wa Bodi za mashirika haya na walahapaswi kushiriki kwenye vikao vya bodi vya mashirika haya kwaniyeye ni msimamizi mkuu wa mashirika hayo na anapaswa kusimamiautendaji kazi wake.
Mheshimiwa Spika, pamoja na mabadiliko hayo ya sheria badomsajili wa hazina amekuwa akihudhuria vikao mbalimbali vya bodiza Mashirika ya Umma kama mjumbe jambo ambalo ni kinyume nasheria, na amekuwa akishiriki moja kwa moja kwenye maamuzi yabodi hizo jambo ambalo linamfanya kushindwa kutimiza wajibuwake wa kuwa msimamizi kama ambavyo sheria inaelekeza.
Kambi ya Upinzani inataka kupata maelezo ya kina ni kwa nini halihii imeendelea kuachwa iwe ilivyo kwa msajili wa hazina kuendeleakuwa mjumbe wa vikao vya Bodi za mashirika ya umma kinyume nasheria. Aidha tunataka kauli ya serikali kuhusiana na suala hili.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inapenda kupata maelezo yaSerikali kuhusu masuala yafuatayo.Moja, Sakata la uuzwaji wa hisa za Shirika la UDA umefikia wapi?Pili, Serikali imefikia wapi katika utungaji wa Sheria mpya ya Ofisi yaMsajili wa Hazina ili kuimarisha usimamizi wa Mashirika ya Umma.Tatu, Serikali imefikia wapi katika pendekezo la kuifanyiamarekebisho Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC) ili liwezekumiliki, kusimamia na kuziendesha hisa za serikali katika Kampunibinafsi ambapo umiliki wa Serikali ni chini ya asilimia 50. Pendekezohili lilikuwa ni uamuzi wa Bunge na hivi sasa mwaka mzima umepitabila Bunge kupatiwa taarifa yeyote kinyume na maelekezo yake.Nne, Serikali imefikia wapi katika utekelezaji wa Waraka nambamoja wa mwaka 2012 kuhusu usimamizi na uendeshaji wa Mashirikaya Umma na hasa mahusiano kati ya Mashirika ya Umma na Wizaramama. Waziri wa Fedha kama msimamizi mkuu wa Mashirika ya Umma amechukua hatua gani kuhakikisha falsafa ya ‘eyes on,hands off’ katika kusimamia Mashirika ya Umma inatekelezwa kikamilifu na kuhakikisha Mashirika ya Umma yanaendeshwa kwafaida na bila kuingiliwa ingiliwa na Wanasiasa?
7.0 Ofisi ya Takwimu ya Taifa
Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (National Bureau ofStatistics NBS) ilizinduliwa rasmi tarehe 26 Machi, 1999 kamaWakala wa Serikali (Executive Agency) kwa mujibu wa Sheria yaWakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997, (The Executive AgenciesAct 1997) (Act No. 30 of 1997), na ndio chombo rasmikinachojihusisha na kutafuta, kuandaa na kusambaza takwimuhapa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, katika kupanga mipango ya maendeleo nakuandaa sera mbalimbali za nchi husika, upatikanaji wa takwimurasmi zinazotokana na Kanuni na Mbinu za Kitaalamu iliyowekwa naOfisi ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa (United Nations StatisticalDivision) ni muhimu. Takwimu zote zilizo rasmi duniani hutolewa naOfisi za Takwimu za nchi husika kupitia Sheria za Takwimu za nchimbali mbali.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani imekua ikitoaMapendekezo ya kuboresha utendaji wa Ofisi ya Takwimu katikaNyanja mbalimbali na serikali kutothubutu kuchukua mapendekezohayo na kuyafanyia kazi.
Mheshimiwa Spika, katika taarifa ya miaka hamsini ya wizara,taarifainaonesha wizara kuwa na nia ya kuboresha ofisi ya takwimu yataifa kwa kuboresha miundombinu ya utoaji takwimu nchini,kuimarisha mfumo wa takwimu nchini (NBS), kutoa takwimu sahihina kwa wakati, kutokana na nia hii ya serikali Kambi Rasmi yaUpinzani inaitaka serikali kuzingatia Ofisi ya Takwimu Kuwa nauhisiano wa moja kwa moja wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa na ngaziza Mikoa, Halmashauri za Wilaya, Kata na Vijiji kurahisisha upatikanajiwa takwimu ili zisaidie katika kupanga mipango ya maendeleo.
8.0 Mamlaka Ya Mapato-TRA
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekezakwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania ijenge uwezo wa kukaguamahesabu ya kikodi kwenye Kampuni za Utafutaji wa Mafuta naGesi, Kampuni za Madini na Kampuni za Simu ambazo uzoefuunaonyesha kuwa katika maeneo haya kuna mbinu nyingi sana zakukwepa kodi.
Mheshimiwa Spika, kwa msisitizo mkubwa sana Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inaitaka mamlaka ya Mapato Tanzaniakushirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Mawasiliano nchini kukaguamapato ya Kampuni za simu na hasa kampuni ambazo zinatoahuduma kwenye kampuni za Simu.
Mheshimiwa Spika, Katika mjadala wa Bajeti ya Wizara yaMawasiliano kulikuwa na mjadala kuhusu namna ambavyo wasaniiwa Tanzania wanavyonyonywa mapato na Kampuni zinazotoahuduma ya miito kwenye kampuni za simu. Bunge lako lilielezwakwamba Biashara ya miito kwenye simu ina thamani ya shilingi bilioni43 kwa mwaka lakini msanii anayetengeneza kazi zinazouzwaanapata asilimia 7 tu ya mapato hayo.
Mheshimiwa Spika, taarifa zaidi za ziada zinaonyesha kuwa kampuniya On Mobile yenye mkataba na Kampuni za Simu za Vodacom na Airtel kama ‘aggrigator’ wa miito ya simu yenye miziki ya wasaniihapa nchini hailipi kodi kutokana na mapato yake. Kambi Rasmi yaUpinzani inaitaka Serikali kutoa taarifa za kikodi za kampuni hii nawashirika wake na hatua ambazo Serikali imechukua dhidi yao.Kambi ya upinzani inashauri pia kwamba Mapato yanayotokana na miradi kama hii kwenye Kampuni za simu yawe ‘ring fenced’ na kutozwa kodi stahiki au kodi maalumu.
9.0 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani-Internal Auditor General
Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mkuguzi Mkuu wa Ndani (Internal Auditor General) iliyoanzishwa na mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya mwaka2010 inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwazikileta migongano katika maeneo ya kiutendaji na uwajibikaji,sheria haipo wazi juu ya upatikanaji wa mtaalam huyo kamainavyotakiwa na sheria na 8 ya utumishi wa umma, kwa mfanokutangazwa kwa nafasi hizo na waombaji kufanyiwa usaili.
Mheshimiwa Spika, pamoja na utata wa uteuzi wa mkaguzi wandani kama sheria ya utumishi wa umma inavyoelekeza mkaguzi wandani anasimamiwa na Katibu Mkuu Hazina (Paymaster General) ambaye naye ni mkaguliwa- kwa hiyo kunakuwa na mgongano wakimaslahi uhuru wa ofisi ya mkaguzi wa ndani inaweza kukosa uhuruKambi Rasmi ya Upinzani inaishauri serikali katika ofisi ya Mkaguzi waNdani (Internal Auditor General office) ingepaswa iwe na bodiambako maalumu wangekuwa wanaripoti ili kuweka uhuruunaofaa.
Mheshimiwa Spika, wakaguzi wa ndani ni waajiriwa wa serikali nahufanya kazi zao za ukaguzi kwa kipindi chote ambacho shughuli zaserikali zikifanyika, mfano; katika halmashauri wakaguzi hutakiwakuwajibika kuanzia upokeaji wa fedha kutoka hazina, hadi kutumikakwake, Kambi Rasmi ya Upinzani inahoji serikali nini nafasi yawakaguzi wa ndani kama ubadhirifu wa fedha za ummaumeendelea kuwepo kama ripoti za mkaguzi mkuu wa hesabu zaserikali zinavyothibisha?
Mheshimiwa Spika, katika ushughulikiaji wa matumizi mabovu yarasilimali za umma serikali imekuwa legelege hasa pale taarifa zinapotolewa na wakaguzi wa ndani ambao hutoa taarifa marakwa mara na seriakali kukaa kimya, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka serikali kutambua umuhimu wa taarifa hizi za wakaguzi wandani na kuhakiki inachukua hatua stahiki pasipo kusubiri taarifa zamkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambazo ukaguzi wakehufanyika kwa kuchelewa zaidi.
10.0 Utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012 Pamojana Mpango wa Maendeleo kwa Mwaka 2012/2013
Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya Wizara ya Fedha mwaka2011/2012 fungu Namba 50wizara ilitenga shilingi bilioni 659 kwaajili ya miradi ya maendeleo na fedha zilizotumika hadi kufikia Juni2012 ni shilingi bilino 402.7 ambapo fedha za ndani zikiwa shilingibilioni 78.65 sawa na asilimia 11.9 ya bajeti ya maendeleo hivyokutegemea fedha za nje katika kutekeleza miradi ya maendeleokwa asilimia 88.1. Kambi Rasmi ya Upinzani, pamoja na Serilialikutokubali kutumia mapato ya ndani zaidi katika kugharimia miradiya maendeleo, I azidi kushauri serikali kuwa na Makati wa dhati wamuda mrefu wa kuachana na utaratibu wa kutegemea misaada yanje. Mkakati huo ulenge kuiongezea mapato kwa kutumia mbinumbalimbali za kodi.
Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya 2012/2013 serikali imetengashilingi bilioni 546.51 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ni pungufu kwa asilimia 18 ya bajeti ya mwaka 2011/2012ambapo serikali ilitenga shilingi bilioni 659. Katika bajeti ya 2012/2013ni asilimia 19.3 tu ya fedha za ndani ndizo zimeelekezwa kwenyemiradi ya maendeleo na asilimia 80.7 ya makadirio ni fedha za njeikiwa ni mikopo ya kibiashara na misaada. Kambi Rasmi ya Upinzaniinahoji: ni maendeleo yapi ambayo serikali inadhamiria kwakutenga fedha ya maendeleo ambayo ni pungufu kwa asilimia 18ya bajeti ya mwaka jana?
HitimishoMheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inasisitiza umuhimuwa kuisimamia vema Wizara ya Fedha katika kusimamia uchumi wanchi. Tuna imani kwamba Waziri wa Fedha ndugu William Mgimwana Manaibu wake Mhe. Janeth Mbene na Mhe. Saada MkuyaSalum wataweza kukabili changamoto tulizoainisha katika hotubayetu na kufanyia kazi mapendekezo ambayo tumeyatoa. Tumeonadalili za Wizara hii na hasa Waziri na Manaibu wake kusikiliza katikamasuala ya Kikodi hivyo, tuna imani kwamba wataendelea kusikiliza.

Kambi Rasmi ya Upinzani haitasita kutoa ushirikiano kwa lengo lakuleta maendeleo katika nchi yetu. Hata hivyo, tutakosoa kwanguvu zetu zote na kuchukua hatua za kiuwajibikaji dhidi ya njamazozote za kudhoofisha maendeleo ya Taifa na watu wake. Siku zotetutasimama upande wa wanyonge na kuwasemea wasio na sauti,Watanzania milioni 30 wanaoishi vijijini na kwenye dimbwi laUmasikini (The Bottom 30M).
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo kwa niaba ya KambiRasmi ya Upinzani naomba kuwasilisha.
……………………………………

 Kabwe Zuberi Zitto (Mb)
Waziri Kivuli-Wizara ya Fedha
12.08.2012

KIAMBATANISHO A.
Sheria mbalimbali kuhusiana na fedha haramu
i.the establishment of the Permanent Commission of Inquiry, or Ombudsman, 1966;
ii.the Foreign Exchange Control Act 1966;
iii.the Anti-Corruption Act 1971;
iv.the establishment of an anti-corruption squad in 1975;
v.the Economic Sabotage Act 1983;
vi.the Economic and Organised Crime Act 1984;
vii.the Proceeds of Crime Act 1991;
viii. the Leadership Code (Declaration of Assets) Act 1995;
ix.the appointment of the Presidential Commission of Inquiry into Corruption,1996;
x.the BOT Circular to Banking and Non-banking Financial Institutions, No. 8of 2000, on Money Laundering.
xi.the Drugs and Illicit Traffic of Drugs Act 1995;
xii. the Arms and Ammunition Act 1991;
xiii.the Mutual Assistance in Criminal Matters Act 1991; and
xiv.the Tanzania Intelligence and Security Act 1998.
xv.The anti-money laundering Act, 2007
xvi.the anti-money laundering (amendment) act, 2012.

No comments:

Post a Comment