Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, August 11, 2012

HUU NDIO MUONEKANO MPYA WA WA KING JOFA BLOG,,, UKIWA KAMA MDAU MUHIMU SANA KWENYE BLOG HII UNAKARIBISHWA KUTOA MAONI YAKO...!

Habari? 
Nawashukuru sana wadau wote mlio tembelea Blog yangu ya KING JOFA, kwa muda wote bila kuchoka pia natanguliza kusema natambua mchango wenu mkubwa sana katika kuniwezesha kwa kunitumia habari na matukio mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine yaliwavutia watu wengi  kuisoma Blog hii. Nimeamua kuibadilisha Jina na muonekako wa Blog hii lengo likiwa ni kuitoa katika umiliki wa mtu binafsi na kuifanya iwe fahari ya kila mmoja wetu kuwa huru katika kutoa mchango wake wa Mawazo, Habari, Matukio na mchango mwingine wa aina yoyote ili kuleta mafanikio na mabadiliko ya mtazamo chanya katika jamii. Na nilijitahidi kufikiria jina kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kukusanya maoni kutoka kwa wadau tofauti tofauti na kuamua kuipa Blog hii jina la "KILIMANJARO OFFICIAL BLOG" dhumuni likiwa ni kuupa mlima huu heshima ya juu na kuzidi kuutangaza kote ulimwenguni..

 
 Picha hii inaoyesha Jina na Muonekano wa mwazo wa "KING JOFA BLOG" ila kwa sasa umebadilika.

 
 Picha hii ndio inaonyesha Jina na  Muonekano mpya ambayo kwa sasa ni "KILIMANJARO OFFICIAL BLOG".

Tunaheshimu karibisha maoni ya wadau wote katika kujenga blog yetu.. Je unamtazamo gani juu ya muonekano mpya wa Blog hii..
Unaweza kuandika comment zako hapo chini na comments zote tutazifanyia kazi na kuwapa majibu...
Tunatanguliza shukrani za dhati kwa mchango wenu mkubwa maana bila nyie tusingeweza kufika hapa tulipo..

No comments:

Post a Comment