Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, August 10, 2012

JINAMIZI LA AJALI LAENDELEA KUIANDAMA TZWatu 15 ambo ni Raia wa Kenya wanasadikiwa kufariki Dunia Mpaka sasa na wengine 22 kujeruhiwa.
Ajali hiyo inaripotiwa kutokea mnamo Saa kumi na Moja asubuhi katika Eneo La Mto Wami ambapo ajali hiyo ilihusisha Magari manne.

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Bw Mohamed Mpinga alielezea Chanzo cha ajali hiyo ni kuwa Gari mbili za Abiria zilizokua Zimebeba Raia wa Kenya Ambao ni waumini wa Kikristo waliokuwa wakielekea Dar es Salaam kwa shughuli  za kidini Ghafla gari yao Moja iliyoko mbele ikapatwa na pancha iliyopelekea Kutaka kutokea ajali ila Dereva akaigotesha gari pembezoni Mwa Barabara ambapo dereva wa Gari ya Pili akapaki ili watoe Msaada.

Wakati Wanatoa Msaada Msaada Ilitokea Gari aina ya Lori iliyokua ikitokea Tanga Ndipo  ikaigonga Ile gari iliyokua imepaki Pembeni.

Baada ya Ajali hiyo Gafla ikatokea Lori jingine Lililokua likitokea Dar es Salaam na Kugonga Lile Lori lililokua limegonga ile gari.

Majeruhi walipelekwa Katika Hospitali ya Tumbi kwa Matibabu wakati Maiti walihifadhiwa katika Hospitali hiyo na Taarifa kutoka kwa Walio kuwa katika hilo gari kuwa waliopoteza Maisha wote ni Raia wa Kenya.

No comments:

Post a Comment