Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa tai nyekundu),akimtambulisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (aliyenyoosha mikono)Mhandisi Madeni Kipande,mchana huu alipotembelea Bandari hiyo.Waziri wa Uchukuzi wa Uchukuzi amewasimamisha kazi Mameneja wa Bandari ya Dar es Salaam,Meneja wa Kurasini Oil Jet(KOJ),Meneja wa JET,Mhandisi wa kituo cha Mafuta(Oil Terminal Engineer),Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari(TPA),na Wakurugenzi Wakuu Wasaidizi wawili wa Mamlaka hiyo kupisha Uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazoikabili Mamlaka hiyo.

Waziri wa Uchukuzi,Harison Mwakyembe(aliyesimama)akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), mchana huu wakati akiwataka kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.

Sehemu ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi,hayupo Pichani,wakati alipowatembelea leo mchana na kuwaeleza dhamira yake ya kuongeza ufanisi katika utendaji wa Mamlaka hiyo.