Anaitwa
Abdullah Juma Abdalla Saddallah na familia yake kupata ajali mbaya eneo
la Tumbi Kibaha wakati akitoka Bungeni na familia yake.
Ajali
hiyo mbaya ilitokea majira ya jioni hii wakati naibu waziri huyo
akitokea Bungeni kuelekea jijini Dara es salaam akiwa na mkewe pamoja na
watoto wake wawili na a dereva wake ambaye aliumia vibaya na kukimbizwa
hospital yaTumbi-Kibaha Mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo Abdulaziz Video
amedai kuwa chanzo cha ajali hiyo inasemekana alikuwa analikwepa Lori
alilokuwa akipishana nalo na hivyo gari lake kuhama njia na kupinduka. Imeelezwa
baada ya ajali hiyo umati wa wananchi wakiwemo vibaka walifika eneo
hilo kutaka kupora mali mbali mbali ila hawakuweza kufanikiwa baada ya
raia wema kusaidia kuepusha hali hiyo .
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo baada ya kuhojia na mwandishi wa habari hizi na kuwa hali ya naibu waziri huyo si mbaya sana zaidi ya dereva wake ambaye ameumia kichwani.".

Chanzo: Francis Godwinblog.
No comments:
Post a Comment