Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, August 13, 2012

NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO MJINI MOSHI


Gari la kikosi cha zimamoto likiwa eneo la tukio

Moto mkubwa Umeibuka katika nyumba iliyoko Eneo la Majengo mjini Moshi na kusababisha Hasara kubwa.Tukio hilo limetokea Leo Mnamo wa Saa nane na robo Mchana Baada ya Kutokea Hitilafu ya Umeme iliyosababisha Mlipuko mkubwa wa Moto.

Wakati tukio hilo linatokea Wapangaji wanaoishi katika nyummba hiyo walikua Kazini nyumba haikua na Mtu Hapo ndipo jitihada za kudhibiti Moto huo zilipanza kuchukuliwa na Wananchi kwa kutoa tarifa kwa kikosi cha Zimamoto na kuja kushirikiana na Wananchi lakini haikuwezekana kuuzima Moto huo mara Moja.

Majirani wakijaribu kuokoa baadhi ya vitu vilivyosalia

Mwenyekiti wa Mtaa wa eneo hilo anayefahamika kwa jina moja tu la Mama Sabitina alisema Kikosi cha zmamoto kilifika kwa muda ila tatizo ni kuwa Moto ulikua ni mkubwa sana na umeme ulikua bado haujazimwa kwa hiyo bado kulikua na shoti katika nguzo ya umeme iliyokua karibu na nyumba hiyo. Nyumba hiyo Mali ya Mzee koshuma yenye jumla ya Wapangaji wanne moto uliwea kuzimwa baada ya dakika 45 lakini hakuna kitu kilichoweza okolewa kwani kvitu vyote viliteketea kwa Moto.

Nyumba inavyoonekana baada ya Moto kuzimwa.

Mpaka tunaondoka eneo hilo hakukua na idadi rasmi ya gharama za Mali zilizoteketea kwa kuwa wapangaji wengine walikua hawajafika bado eneo la tukio kwa kuwa walikua bado Makazini.

No comments:

Post a Comment