Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 16, 2012

Sakata la Kupanda kwa Ushuru wa magari ya abiria Standi ya Moshi bado linaendelea...!

Mkurugenzi wa manispaa ya moshi mkoani Kilimanjaro, Bernadette Kinabo
amewataka madereva wanaoingiza magari yao katika stendi kuu ya mabasi
moshi kulipa ushuru uliongezeka na kuacha kulumbana kwa kuwa kiwango
kilichoongezwa hakita badilishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na
madereva wanaoingiza magari katika stendi na kukataa kulipa ushuru kwa
madai kuwa ushuru huo umeongezwa bila kushirikisha madereva hao,
Kinabo amesema kiwango hicho hakitabadilishwa na wanatakiwa kulipa ili
manispaa iweze kujenga barabara zote kwa kiwango cha lami.

Kinabo amesema madereva hao wanakataa kulipa kutokana na wakala
aliyepewa tenda ya kukusanya ushuru ndani ya manispaa hiyo kushindwa
kusimamia zoezi la kupanga magari na kukusanya ushuru huo.

Mkurugenzi huyo amesema zoezi hilo limekwama kutokana na wakala
aliyepewa tenda hiyo kushindwa kupanga magari na kutoza ongezeko hilo
na kwamba manispaa inaweka wakala mwingine ambaye ataweza
kusimamia zoezi la kutoza viwango vya ushuru vilivyoongezeka.
 
Nao baadhi ya madereva hao ambao ni Daniel Kimwaga, Muhamed bonge
na Mwidoe Rajabu wamesema hawatalipa kiwango hicho na badala yake
watalipa kiwango cha zamani ambacho walichokubalina na manispaa hiyo
kutokana na manispaa kutowashirikisha madereva hao kuhusiana na
mabadiliko ya ushuru huo.

No comments:

Post a Comment