Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, September 16, 2012

AFUNGWA MIAKA 15 KWA KUKUTWA NA MABOMU NA RISASI...!

Mahakamaya Wilaya Kigoma imemhukumu James Nyakamwe (65) kutumikia kifungo cha  miaka 15  jela  kwa kosa la kupatikana na mabomu mawili ya kurusha kwa mkono na risasi nane za SMG.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu George Buyamba baada ya mshtakiwa kukiri kosa.

Hakimu Buyamba alisema kuwa, mahakama hiyo inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwake na vijana wengine wenye tabia ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Awali akisoma hati ya mashtaka Inspekta wa polisi Jonas Kakwaya, alidai kuwa Septemba 11, mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika kitongoji cha Mpeta Kijiji cha Malagaras Wilaya ya Uvinza mkoani  Kigoma mshtakiwa alikamatwa na mabomu mawili ya kurusha kwa mkono pamoja na risasi nane za SMG  kinyume cha sheria.

No comments:

Post a Comment