Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, September 4, 2012

Apigwa Kichwani hadi kupoteza Maisha akiwa bar...!

Mtu mmoja ameuawa  katika kijiji cha  Ketasakwa  kata ya Bwiregi Tarafa ya Kiagata Wilaya ya Butiama mkoani Mara baaba ya kupigwa katika ugovi ambao umetokana na ulevi.
 
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mara Kamishina Msaidizi Mwandamizi  Absalom Mwakyoma,amemtaja mtu huyo ni Maswe Kihenge mwenye umri wa miaka 26 ambaye alipigwa na kitu kizito kichwani na Shera Wasaga mkazi wa kijiji hicho.
 
Amesema tukio lilitokana na Ugomvi uliokuwepo kati yao katika Klabu ya Pombe za Kienyeji ambapo baada ya tukio hilo mtu huyo alikimbizwa katika kituo cha Afya Kiagata kwa Matibabu lakini alifariki dunia baadaye.
 
Kamanda Mwakyoma amesema kuwa Mwili wa Marehemu ulifanyiwa Uchunguzi na Daktari na baadaye kukabidhiwa kwa ndugu wa Marehemu kwaajili ya Mazishi.
 
Hata hivyo amesema kuwa mtuhumiwa Shera Wasaga anatafutwa baada ya kutoroka baada ya Tukio hilo.
 
Kwa sababu hiyo kamanda Mwakyoma ametoa wito kwa Wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi na kuepuka Ulevi wa Kupindukia.

No comments:

Post a Comment