Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, September 4, 2012

Shule tano za Msingi zanufaika na Chakula cha Msaada...!

Jumla ya shule tano zilizopo katika kata tatu za manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro zimenufaika kwa msaada wa chakula cha mahindi zaidi ya tani sita na maharage zaidi ta tani moja  vikiwa na thamani ya sh 5.5mil kutoka katika shirika lisilo la kiserekali la Nuru kwa watu  wote lenye makao yake makuu nchini Marekani

Msaada huo umekabidhiwa jana na mkurugenzi wa shirika hilo Bw.Ran Barr kwenye hafla fupi iliyofanyika katika shule ya msingi Azimio iliyopo katika kata ya Boma mbuzi manispaa ya Moshi ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini zote,viongozi wa kisiasa na waalimu wakuu wa shule hizo

Bw, Barr amesema msaada huo wameutoa baada ya kupata maombi kutoka kwa viongozi wa manispaa hiyo kuwa kuna zaidi ya shule 12 zenye matatizo mbalimbali  ikiwemo vifaa vya shule na ukosefu wa  chakula cha mchana kinachosababisha wanafunzi kuwa watoro na kutokuwa wasikivu  na kuamua kuzisaidia shule tano na kuendelea na shule nyingine kwa awamu nyingine.

Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Moshi ambae pia ni diwani wa kata ya boma mbuzi Mh. Jafar Michael ameshukuru kwa msaada huo na kusema utawasaidia watoto hao kuendelea vyema na masomo yao hususani watoto wenyekutoka katika familia zisizo na uwezo na kuwataka watu wote wenye mapenzi mema kuwasaidia watoto kwa hali na mali na sio kungojea wafadhili kutoka nje.

Mh. michael amezitaja shule hizo ni pamoja na shule za msingi Azimio, Mandela, Pasua, Msaranga na shule ya msingi Msandaka zote zikiwa ziko katika manispaa ya moshi

No comments:

Post a Comment