Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, September 13, 2012

CHAMA CHA WALIMU TANZANIA CHAPENDEKEZA KWA SERIKALI NAMNA NZURI YA KUMALIZA MGOGORO BAINA YAO...!

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mwl. Gratian Mukoba (kushoto) akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya mapendezo ya Chama hicho kwa serikali ya namna ya kumaliza mgogoro baina yao. Amesema Chama kinaamini kuwa serikali itapokea ushauri wa CWT.

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa mara nyingine kimetoa taarifa kuhusu mapendekezo ya chama hicho kwa serikali juu ya namna nzuri ya kumaliza mgogoro kati ya walimu ba serikali.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Rais wa Chama cha Walimu Mwl. Gratian Mukoba amesema CWT kinatambua kuwa serikali ilidai kuwa ilijadiliana na watumishi wake na kutangaza matokeo ya majadiliano hayo kwenye gazeti la serikali la Julai 2 mwaka huu.
Na kwa tangazo hilo la serikali, walimu wakirudi kujadiliana kwenye Baraza la Majadiliano la Pamoja kwenye Utumishi wa Walimu, majadiliano hayo yatakuwa kwa mwaka ujao wa fedha.
Mwl. Mukoba amesema ili kuwatia moyo walimu na kuwaongezea ari ya kufanya kazi, madai yao yanahitaji kusikilizwa ndani ya mwaka huu wa fedha, hivyo wameishauri serikali kuchukua hatua mbili muhimu.
Amezitaja hatua hizo kuwa Kuteua Timu ya Madiliano na Kusajili Makubaliano kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.

No comments:

Post a Comment