Pichani ni Wafanyabiashara ndogo ndogo za mboga mboga kwenye soko kuu la Arusha wakiwa wamepanga bidhaa zao pembeni ya barabara bila kujali usalama wao na kusababisha msongomano wa magari katika kupishana hali inayokuwa ngumu kwa waenda kwa miguu kwenye barabara hiyo.

ABIRIA CHUNGA MZIGO WAKO SOKO KUU LA ARUSHA…..Mmoja wa vibaka ambaye hakutambuliwa jina lake ambao ni kundi la kuiba simu na fedha mifukoni akiwa amekamatwa na wananchi wenye hasira kwenye soko kuu la Arusha.

Mwananchi akiwa amempiga Tanganyika jeki kibaka huyo aliyekwapua simu ya dada mmoja (hayupo pichani).
Kibaka huyo akiendelea kujitetea kwa wananchi kuwa hajaiba simu na pembeni mwenye fulana ya Orange ni mwenzake kwenye kundi hilo la vibaka.
Pichani Juu na Chini ni Heka heka za kutafuta mahitaji kwa wakazi wa jijini la Arusha jioni baada ya mihangaiko ya mchana kutwa kama ilvyokutwa na Camera yetu jijini Arusha.

Wajasiriamali wakiendelea kusubiri wateja.

Mboga mboga aina ya Kabichi zikiwa zinashushwa katika soko kuu la Arusha kutokea katika kijiji cha Orkokola na Kiding’a wilaya ya Arumeru.

Picha Juu na Chini Serikali ya JK ikionyesha kasi za Ujenzi barabara za jiji la Arusha hapa ni moja ya barabara ambayo ipo katika hatua za mwisho kabla ya kuwekwa lami na hii ni moja ya barabara mbalimbali za jiji hili zilizopo katika mpango wa uwekaji wa lami picha kama zilivyokutwa na Camera yetu jijini Arusha.