Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, September 9, 2012

Tisa wakamatwa bandarini Dar wakipakua Shaba

"Mwakyembe ang`aka, washitakiwe"
Watu tisa akiwemo askari polisi wa kituo cha Tazara jijini Dar es Salaam, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Bandari, baada ya kukamatwa wakipakua madini ya shaba kwenye mabehewa usiku wa kuamkia jana.
Tukio hilo limetokea katika bandari ya Dar es Salaam, lakini dereva wa treni iliyobeba shaba hiyo, alikimbia na treni baada ya kufanikiwa kugonga geti na kulivunja huku watuhumiwa wenzake wakitiwa mikononi mwa polisi.
Akizungumza na NIPASHE Jumapili jana, huku akiomba jina lake lisiandikwe gazetini, mmoja wa askari wa kituo cha polisi cha bandari kilichopo Kurasini, alisema tukio hilo lilitokea saa 9 alfajiri baada ya walinzi wa bandari hiyo kuwashitukia watu wakipakua shaba hizo na kupakia kwenye behewa jingine.
“Treni la mizigo liliwasili usiku bandarini likiwa limesheheni shaba, lakini askari wetu walishangaa kuona watu wakipakua toka behewa moja kwenda jingine huku dereva wa treni akizuga kubadili kichwa cha treni yake…lakini baada ya kushitukiwa polisi aliyeongozana na treni hiyo pamoja na wapakua mizigo wakatiwa mtegoni,” alisema mtoa habari huyo.
Hata hivyo, mtoa habari huyo alikataa kutaja majina ya watuhumiwa hao pamoja na polisi aliyekamatwa ingawa NIPASHE Jumapili iliwashuhudia wakipandishwa katika gari la polisi bandari lenye namba PT 0880 Land Rover defender.
Aidha, ilidaiwa shaba waliyokamatwa nayo watuhumiwa hao inakadiliwa kufikia kilo 700 ikiwa na thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni moja.
Mtoa habari huyo alieleza zaidi kuwa shaba hiyo iliyotoka nchini Zambia, ilitakiwa kushushwa katika bandari ya Dar es Salaam, kisha mabehewa ya treni hiyo yapakiwe mbolea ambayo ingepelekwa nchini humo.
Hata hivyo, gazeti hili lilipojaribu kuwasiliana na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Mhandisi Madeni Kipange aliyekuwa kituo cha polisi bandari Kurasini, hakutaka kuzungumza chochote licha ya kuzungukwa na wanahabari na badala yake alipanda gari lake na kuondoka.
Ilisemekana, mkurugenzi huyo ameitwa pamoja na mwenzeke wa Tazara ofisini kwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuzungumzia tukio hilo.
Waziri Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, akiongea na waandishi wa habari jana baada ya kutokea tukio hilo, aliagiza watu wote waliohusika na wizi huo na kukamatwa wafunguliwe mashitaka.
Alisema Afisa wa bandarini aliyehusika kufunga kontena Namba MSKU 268357(6) ameshafahamika na y eye atakamatwa ili afunguliwe mashitaka.
Akizungumzia wizi ulivyotokea, Dk. Mwakyembe alisema usiku wa kuamkia jana kulitokea matukio mawili ya wizi ambapo la kwanza lilitokea saa 9 usiku ambapo injini ya treni yenye kichwa Namba CK620006 ilikuwa inakwenda bandarini kwa ajili ya kubeba mabehewa nane.
Alisema kati ya hayo, nane yalibeba mbolea na matatu yalikuwa tupu.
Alisema katika treni hiyo kulikuwa na wafanyakazi wanne ambao ni dereva Abdallaham Shebe, muongoza treni Bakili Kitanda, Polisi PC Abubakar mwenye namba F8784 na msimamizi wa treni Gideon Anyona.
Dk. Mwakyembe alisema wakiwa bandarini walivunja kontena ambayo ilikuwa na shaba na kuanza kupakua na kuihamishia kwenye makontena ya treni ya Tazara na kufanikiwa kuhamisha vipande 19.
Wakati wakiendelea na harakati hizo. Kulizuka mapambano kati ya polisi na wafanyakazi hao ambapo dereva pamoja na muongozaji walifanikiwa kukimbia na kwenda eneo la Yombo na wengine wawili walikamatwa.
Katika tukio la pili lililotokea saa 10 alfajiri jana katika depo la Oryx kulikuwa na kundi kubwa la watu waliokuwa wanaiba madumu ya mafuta kutoka kwenye depo hiyo na kuyatupia upande wa pili wa bandarini. Madumu yalikuwa tisa ya lita 20 kila moja yalikuwa na petroli.
Alisema wakati wanaendelea na harakati hizo polisi waliokuwa doria walifika eneo la tukio na kukuta polisi wa bandarini wakipambana na kundi la wezi lakini polisi wa doria badala ya kuwasidia polisi wa bandarini kupambana na wezi hao, walianza kuiba madumu hayo ya mafuta na kuchukua manne na kuondoka nayo.
Katika tukio hilo watu wanne wamekamatwa.
Alisema askari waliokuwa kwenye doria wanatafutwa .
Aidha, alisema bosi aliyewatuma wafanyakazi kuiba shaba kwenye kontena anaonekana kuwa ni mzoefu kwa hiyo watakamkamata kwa sababu wameshamfahamu.

No comments:

Post a Comment