Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, September 16, 2012

WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE WAASWA KUJIHUSISHA NA VITENDO VIOVU...!

Wahitimu kidato cha nne shule ya sekondari Singida, wakiwa wamepozi ktk mahafali ya 11 ya shule hiyo yaliyofanyika jana
Mwanafunzi kidato cha nne shule ya sekondari Singida, Marystella Makungu akilishwa keki na mama yake, Bi.Hellen Bogone
Baadhi ya walimu wa shule hiyo kutoka kulia mbele ni Mwl. Mutta Anselimi, Ester Kimaro,Imori Marwa na mkuu wa shule hiyo

VIJANA wanaomaliza kidato cha nne kwenye shule mbalimbali za sekondari nchini wameasawa kujiepusha na vitendo viovu ili pamoja na mambo mengine kuepuka maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI.


Katibu Idara ya utumishi wa walimu Mkoa wa Singida Samwel Ole Saitabahu alitoa rai hiyo kwenye mahafali ya 11 ya wahitimu 56 wa Kidato cha nne, shule ya Sekondari Singida.

Alisema kuwa vijana wengi baada ya kukosa nafasi za kuendelea na masomo ya juu wanakata tamaa na kujiingiza katika wizi, ukahaba, utumiaji madawa ya kulenya, ulevi, ubakaji na ulawiti.


Saitabahu alisema kuwa, licha ya kufungwa jela, kuuawa na wananchi mwenye hasira kali, wanaweza kuambukizwa virusi vya UKIMWI, hata kuuawa na kupoteza kabisa ndoto za maisha yao ya baadaye.

Kutokana na hali hiyo, amewataka vijana kujiendeleza zaidi kimasomo badala ya kukata tamaa ikiwemo kutumia fursa ya kujiunga na vyuo vya ufundi stadi ili kupata taaluma zitakazowawezesha kuajiriwa au kujiajiri kwa kutumia fursa watakazopata.


Na: Elisante John, Singida

No comments:

Post a Comment