Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, September 23, 2012

WAREMBO WAMTOSA DIAMOND KATIKA USAILI WA VIDEO YAKE MPYA...!

 
Tofauti na matarajio ya wengi kwenye usaili wa video mpya ya Diamond Platnumz uliofanyika leo Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam, wasichana wachache wamejitokeza.
 
Akiongea na chanzo chetu cha habari  kwa simu, mmoja wa majaji wa usaili huo Raqey Mohamed wa I-View Media, amesema hakutarajia kuona wavulana kuwa wengi zaidi kuliko wasichana.

Alisema sababu anaziona kusababisha muitikio hafifu wa wasichana ni kutokana na fani ya uigizaji kuwa na sifa mbaya katika jamii, hali inayopelekea wengi kuidharau.

Kufuatia hali hiyo, Raqey amesema usaili huo umefanikiwa kwa asilimia 65 na anasema ni ngumu kumpata ‘muigizaji mkuu wa kike atakayeonekana kwenye video hiyo japo upo uwezekano wa kumbadilisha na kumpa uhusika huo.

Amesema takriban vijana 250 walijitokeza kwenye usaili huo ambapo wamechagua wavulana 20 na wasichana 20 ili kuchuja wale bora watakaoonekana kwenye video hiyo.

Kuhusu muda wa kufanyika kwa video yenyewe, Raqey ambaye ataiongoza amesema bado wanashughulikia masuala ya permit na pindi yatakapokalimika video itaanza kufanyika ndani na nje ya nchi ambapo watasafiri na baadhi ya waigizaji akiwemo lead actress.


Raqey amesema bajeti ya video hiyo inafikia milioni 30 hadi 40.

No comments:

Post a Comment