Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, September 19, 2012

WASIMAMIZI WA MTIHANI WA DARASA LA SABA TAHADHALISHWA...!

WASIMAMIZI  369 Wilayani Tarime  Mkoani Mara wanaotarajia kusimamia mitihani ya wanafunzi wa darasa la saba itakayoanza  jumatano  na Alhamisi ya wiki hii wametakiwa kusimamia mitihani kwa kuzingatia  taratibu za uendeshaji mtihani na kwamba kwa yeyete atakayeenda kinyume  au kubainika kuonyesha wanafunzi majibu atachukuliwa hatua kali za kisheria.
 
Akiongea na V.FM ofisini kwakwe Ofisa Elimu wa Wilaya ya Tarime Emanuel Jonson amesema kuwa  endapo wasimamizi wa mitihani wakisimamia vyema  itasaidia kupunguza tatizo la wanafunzi ambao wamekuwa wakifutiwa mitihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kuonyeshwa  na kuonyeshana majibu.
 
Jonson amesema kuwa  katika mtihani wa mwaka jana kwa shule za Serikali jumla ya wanafunzi 59 kati yao wavulana 22 na wasichana 37 walifutiwa mtihani wa darasa la saba huku wanafunzi wa shule Binafsi  63,wavulana 34 na wasichana 29 nao walifutiwa na kwamba  wote wanatarajia kurudia mtihani huo utakaoanza siku ya jumatano.
 
Jonson amesema  kuwa Wilaya ya Tarime ina jumla ya shule za mshingi 128 ambapo shule za Serikali ni 121 binafsi 7 Nakwamba  jumla ya watahiniwa wote wa shule za Serikali na binafsi  zipatazo 128  kwa Wilaya nzima watahiniwa   wapatao 8146 wavulana wakiwa 4001 na wasichana 4145 watafanya mtihani.

No comments:

Post a Comment