Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 25, 2012

Afya ya majeruhi ajali ya ndege JWTZ yaimarika..!

Majeruhi wa ajali ya ndege ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyopata hitilafu juzi katika makao makuu ya kambi ya Jeshi la Anga, jijini Dar es Salaam anaendelea vizuri.

Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, alisema jana kuwa majeruhi huyo, Kanali Fezuzi Kwiduke, anaendelea vizuri na matibabu katika Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Alisema ndege hiyo yenye namba JW 9129 bado ipo kwenye uwanja ilipopatia hitirafu na ukarabati wake utafanyika siku yoyote.

Ndege hiyo iliyokuwa na marubani wawili wanafunzi ilipata hitilafu juzi muda mfupi kabla ya kuruka na kusababisha kifo cha rubani mmoja aliyekuwapo kwenye ndege hiyo Kapteni Deogratius Magushi.

Makapteni hao walikuwa katika mafunzo ya namna ya kurusha ndege.

Kabla ya kuruka ndege hiyo ilipata hitilafu na kugonga kontena lililokuwa katika kiwanja hicho.

No comments:

Post a Comment