Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 25, 2012

Vita dhidi ya ugaidi yapangiwa mikakati..!

Nchi mbalimbali duniani zimekubaliana kupeana taarifa, pamoja na kusaidiana katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alisema hayo kwenye maadhimisho ya Sherehe za Miaka 67 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN).

Alisema usalama ni jambo muhimu, na kwamba, hiyo ilikuwa ni moja kati ya ajenda kubwa katika mkutano wa kimataifa uliofanyika Geneva nchini Uswisi, ambako alihudhuria na kukubaliana kuwa kuna umuhimu wa kupashana habari katika mapambano dhidi ya ugaidi duniani.

“Bila ya kupashana habari, ni rahisi mtu mmoja kusafiri na kupenya kwenye nchi moja kwenda nyingine, sasa bila kupeana taarifa ni rahisi watu hawa kuleta madhara,” alisema Sitta.

Akizungumzia miaka 67 ya UN, Sitta alisema UNni muhimu sana, na imekuwa na mchango mkubwa katika kuleta na kusimamia amani na utulivu duniani katika kipindi chote cha kuwapo kwake.

Alisema pamoja na kusimamia amani, UN imekuwa ni wa mafanikio, ingawa kuna malengo mengi ya milenia bado hayajafikiwa ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vya watoto, kupunguza umaskini pamoja na njaa.

Naye Alberic Kacou, Msimamizi Mwakilishi wa UN nchini, alisema katika maisha ya sasa changamoto haziepukiki katika kuhakikisha kila mtu anapata mahitaji yake muhimu, ikiwa ni pamoja na ajira kwa vijana, pamoja na kutoa nafasi sawa kwa watu wote hasa wanawake.

No comments:

Post a Comment