Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, October 23, 2012

BINTI ALIYECHOMWA KISU KWA TUHUMA ZA KUIBA MUME WA MTU ARUSHA ATOROKA HOSPITALI HUKU UTUMBO UKINING’INIA...!

Binti aliyekuwa akifanya kazi za ndani Angel Lema (22)mkazi wa Leganga kata ya Usa River wilayani Arumeru, ametoroka wodini katika hospitali alipokuwa amelazwa, akiwa na jeraha kubwa tumboni huku utumbo ukiwa unaning’inia baada ya kuchomwa kisu kwa tuhuma za kukutwa na mume na bosi wake.

Tuhuma za tukio hilo zimethitibishwa na mganga mkuu wa hospitali ya halmashauri ya Meru Dkt. Azizi Msuya na kueleza kuwa awali binti huyo wakati akiletwa katika hospitali hiyo ilielezwa kuwa alijichoma kisu mwenyewe .

Amesema kuwa baadae iligundulika kuwa Binti huyo alichomwa kisu na mke wa bosi wake ambaye polisi bado wanaendelea kumtafuta, baada ya kubainika kuwa alisuka njama za kumtorosha hospitalini majeruhi huyo akishirikiana na mumewe .

Hata hivyo Dkt. Msuya amebainisha kuwa tukio hilo linawahusisha pia baadhi ya polisi wasio waadilifu ambao walishirikiana na watuhumiwa kumtorosha hospitali msichana huyo ili kuficha ushahidi wa tukio hilo.

Dkt. ameeleza kuwa msichana huyo baada ya kufikishwa hospitalini hapo alikuwa katika hali mbaya huku utumbo ukiwa nje kutokana na jeraha kuwa kubwa, na walipomhoji alikana kuchomwa kisu na mke wa tajiri yake badala yake alidai kwamba yeye ndiye alijichoma kwa lengo la kujaribu kujiua.

Aidha amesema wakati wakiendelea kumfanyia matibabu ndipo baadhi ya ndugu walijitokeza na kubainisha kwamba binti huyo alichomwa kisu na mke wa tajiri yake baada ya kumhisi kwamba alikuwa akimwingilia kwenye mapenzi ya mumewe.

Ameongeza kuwa wakati akiendelea kumpatia matibabu ya awali huku akijiandaa kumfanyia upasuaji kesho yake ili kurudishia utumbo uliokuwa ukining’inia ndipo alipopata taarifa kuwa mgonjwa ametoroshwa usiku na watu wasiojulikana

Dkt. Msuya amelalamikia kitendo cha mgonjwa wake kutoroshwa akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kueleza kuwa kuna mchezo mchafu umefanywa na watuhumkiwa wa tukio hilo ili kuficha ushahidi uliokuwa ukihitajika.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas alipoulizwa juu ya tukio hili alithibitisha kupokea taarifa hizo na kudai kuwa ametoa maagizo kwa OCD wa Usa River kumsaka binti huyo ambaye inadaiwa huenda amekilimbilia kwao eneo la Boma Ng’ombe Mkoani Kilimanjaro asaidie upelelezi wa tukio hilo.

Naye OCD Mapujila wa kituo cha polisi Usa River alipoulizwa kwa njia ya simu alisema suala hilo linashughulikiwa na mpelelezi wake ambaye hakumtaja na kueleza kuwa bado hajapatiwa majibu zaidi juu ya tukio hilo.


Na Mahmoud Ahmad-Arusha. 

No comments:

Post a Comment