Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 4, 2012

J.KIKWETE:VIFO VITOKANAVYO NA KUJIFUNGUA HAVIKUBALIKI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Rais Jakaya Kikwete, amesema  vifo vya akina mama vitokanavyo na matatizo ya kujifungua havipaswi kutokea na havikubaliki.

Amesema juhudi zaidi zinahitajika kukabiliana na hali hiyo hasa ikizingatiwa sababu zinazosabisha  vifo hivyo zinazuilika.

“Vifo vya wanawake wajawazito havikubaliki si haki afe wakati akimleta kiumbe mwingine duniani, na cha kusikitisha zaidi wanakufa kwa sababu ambazo zinaweza kuzuilika,” alisisitiza.

Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa  awamu ya pili ya mpango wa ubunifu wa uboreshaji wa huduma ya afya ya mama na mtoto katika maeneo ambayo huduma hiyo haipatikani kwa urahisi nchini.

Uzinduzi wa mpango huo umefanyika mbele ya waandishi wa habari juzi mjini hapa na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki  Moon, Rais Kikwete na wafadhili wakuu wa mpango huo ambao ni Meya wa Jiji la New  York  na Philanthropist, Michael Bloomberg na Dk. Helen Agerup, Mkuu  wa Mfuko wa  H&B Agerup.

Rais Kikwete alisema uboreshaji wa huduma za afya ya mama na mtoto na afya kwa ujumla, ni moja ya vipaumbele vyake muhimu na ni jambo lililo ndani ya moyo wake.

Naye  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki Moon, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania na kutetea haki za wanawake na watoto, amesisitiza haja na umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta za umma na sekta binafsi kuokoa maisha ya wanawake na watoto kwa kuboresha huduma zao.

“Tunahitaji marais,  mameya, wanaharakati wa kuboresha huduma za afya na wafanyakazi wa afya hadi ngazi ya chini kabisa," alisema.

Uzinduzi wa mpango huo ulikwenda sambamba na onyesho la video fupi ya kile kilichokuwa kikifanyika nchini Tanzania, kwa maana ya uokoaji wa vifo vya wanawake wajawazito kwa utoaji wa huduma za dharura za upasuaji baada ya waganga na wakunga kupewa mafunzo ya upasuaji wa dharura.

No comments:

Post a Comment