Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 4, 2012

MWAKYEMBE ATOA MATUMAINI GHARAMA ZA MAFUTA KUPUNGUA

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe

Mtambo mpya wa kupakulia mafuta utakaowezesha meli kubwa za kubeba mafuta yenye uzito wa ujazo wa tani 150,000 kumwaga mafuta na kusafirishwa kwenda kuhifadhiwa kwenye Kituo cha Kupokea Mafuta cha Kurasini (KOJ), utazinduliwa mwezi ujao baada ujenzi wake kukamilika.

Mtambao huo umejengwa katikati ya Bahari ya Hindi, eneo la Mjimwema, Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Meli zitakuwa zinamwaga mafuta kwa kuwa haziwezi kufika bandarini kupakua mafuta kutokana na kina cha maji kuwa kidogo.

Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Franklin Mziray, alisema kazi ya kuufunga mtambo huo ilianza mwaka jana, umefungwa badala ya ule wa zamani uliokuwa ukiwezesha meli ndogo za kubeba mafuta yenye uzito wa ujazo wa tani 35,000 tu.

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Abraham Byandala na Waziri wa Uchukuzi wa Burundi, Moise Bucumi, walifanya ziara ya kuukagua  kwenye mradi ujulikanao kama ‘Single Point Mooring’ (SPM) jana.

Dk. Mwakyembe alisema mtambo buo utaleta mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa mafuta nchini.

“Kwani badala ya meli ndogondogo, ambazo zinakuja kumwaga mafuta KOJ, ambazo zaidi kwa kweli ujazo wa tani wa 35,000, lakini kule kwenye ule mtambo wetu mpya meli kubwa zenye uzito wa tani 150,000 zitakuwa zinamwaga mafuta pale,” alisema Dk. Mwakyembe.

Alisema baada ya kukamilika, kutakuwa na meli kubwa kati ya mbili na tatu zitakazokuwa zikimwaga mafuta kwenye mtambo huo kwa mwezi na kusema mradi huo utasaidia kupunguza msururu wa meli zinazoingia na pia utasaidia kushusha gharama za mafuta nchini.

Alisema mawaziri hao kutoka Uganda na Burundi, wamekuja kujionea mabadiliko ambayo serikali inayafanya hasa katika upande wa sekta ya uchukuzi ili waweze kuitumia zaidi bandari ya Dar es Salaam.  

Akijibu swali lini hasa usafiri wa treni wa Ubungo-Stesheni utaanza, alisema Oktoba 15, kwa kuwa kuna mambo yanayofanywa kuhakikisha usalama wa huduma itakayotolewa kwani hawawezi kukurupuka ili kulifurahish
a gazeti fulani.

No comments:

Post a Comment