Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 11, 2012

MFUKO WA BIMA YA AFYA MKOANI LINDI UMEOWAOMBA WANAHABARI KUIBUA CHANGAMOTO ZA MFUKO HUO...!

Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya umewaomba wanahabari wa Mkoa wa Lindi kuibua changamoto mbalimbali za mfuko huo ikiwemo mafanio na Changamoto zilizopo ili kuboresha huduma za Afya hususani vijijini kufuatia.

Kuongezeka kwa watoa huduma wakiwemo wenye maduka binafsi ya Dawa Akiongea na wanahabari hao mjini Lindi, Msimamizi mkuu wa Nhif Mkoa wa Lindi Fortunata Raymond, alitoa rai hiyo kufuata Urahisi uliopo kwa.

Waandishi kuwafikia wanajamii na kuibua changamoto mbali ambazo zitasaidia Mfuko kuimarika na kuongeza Ufanisi katika kuwahudumia wateja wakiwemo wa mfuko wa Afya ya Jamii CHF Pamoja na hayo alibainisha kuwa Ofisi yake imeanza mkakati wa kutembelea mkoa huo Kata kwa Kata ili kutoa Elimu na kujua mapungufu yaliyopo ambapo waliweza kubaini Upungufu mkubwa wa Watumishi,Dawa na Vifaa tiba.

Aidha walibaini pia Halmashauri walizozifia kutotumia fedha za CHF katika kuimarisha huduma na zingine zikitoa fursa kwa Mwanachama kupata huduma katika kituo alichojiandikisha tu ''Wanahabari naomba muitumie elimu ya leo kuelimisha jamii faida za CHF ili wananchi wengi wa Lindi wajue na kujiunga na mzitumie changamoto nilizowatajia kuikumbusha jamii na mamlaka husika kutekeleza wajibu wao""alimalizia Fortunata.

Akiongea kwa niaba ya Wanahabari akiwashukuru Watumishi wa Nhif kwa kuwatembelea na kutoa elimu hiyo,Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Lindi, Abdulaziz Ahmeid aliiomba ofisi hiyo kuunda vikosi kazi katika ngazi ya wilaya na Mkoa ili kuhakisha kuwa Kaya nyingi zinajiunga na mfuko huo(CHF TASK FORCE)na wanachama wa CHF Wapewe kipaumbele katika kupata huduma  huku ikiimiza Halmashauri kupanga bajeti kwa kazi za CHF Ikiwa pamoja na kuweka kumbukumbu
sahihi za wateja wa CHF/TIKA.
Katika mkoa wa Lindi una jumla ya kaya 194424 na kaya ambazo zimejiunga na mfuko huo ni 10563 sawa na asilimia 5.4

No comments:

Post a Comment