Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, October 11, 2012

UHABA WA KOKOTO WACHELEWESHA KUKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI...!

KUCHELEWA kukamilika kwa mradi  mkubwa wa ujenzi wa  hospitali ya Wilaya Mbarali Mkoani Mbeya kumesabishwa na uhaba wa Kokoto katika Kampuni ya Congolo Mswisswi  ambao ulisimama kwa muda kutokana na Tazara kugoma hivi karibuni.

Imeelezwa kuwa hospitali hiyo ilitarajiwa kukamilika mapema lakini tatizo kubwa likatokea upande wa Kokoto ambazo ililazimika kuagiza Mkoani Kibaha ambako nako walikuwa wakitumia  grama kubwa.

Akizungumza namwandishi wa habari hii ofisini kwake jana Mhandisi wa ujenzi wa Wilaya ya Mbarali Eng.VenatThadei Komba  kuhusiana na ujenzi huo  wa mradi wa hospitali kutokamilika mapema.

Mwandishi  wetu  Esther Macha anaripoti  kutoka Mbeya kuwa ,Eng. Komba alisema mradi huo kwa awamu ya kwanza unategemea kukamilika mwezi wa kumi na mbili na kwamba awamu ya pili wameomba bajeti kwa kwaka huu na kwamba mpaka kukamilika kwake wanategemea kutumia zaidi ya bi.1.5.

“Unajua ndugu mwandishi mpaka sasa kwa hatua hii mpaka kuezeka jingo hili tumetumia zaidi mil.499 na ujenzi unaendelea mpaka sasa”alisema.

Akizungumzia kuhusu changamoto, Eng.Komba alisema vifaa vya ujenzi kama Kokoto  imekuwa shida kiasi kwamba  ilibidi Kokoto ziagizwe Mkoani Kibaha,katika Kampuni ambayo tulikuwa tukinunua ya Congolo Mswiswi hawakuwa wanazalisha wakati mradi huo unaanza kujengwa.

“Kokoto ambazo zilikuwa zinazalishwa zilikuwa kidogo sana kwani sisi tulikuwa tukihitaji tani 40 wakati tukiagiza mswiswi hatupati kiasi hicho ,lakini kuanzia sasa wameanza kuzalisha baada ya mgomo  uliokuwepo hivi karibuni kuisha hali imerudi kawaida”alisema.

Kwa upande wake Ofisa Mipango wa Wilaya ya Mbarali Bw.Elia Mhecha alisema kuwa hospitali hiyo itakapokamilika itahudumia wataanza na wodi ya watoto na wanawake  na baadae itafuata wodi ya wanaume  na kwamba watu wengine ambao watapata huduma hiyo ni Wilaya jirani ya wang’ombe na kuwa mpaka kuisha kwake inategemea kutumia zaidi ya bilioni tatu.

No comments:

Post a Comment