Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, October 6, 2012

POLISI KUWACHUNGUZA WALIO WALINDA MAABUSU WALIO TOROKA

Wakati polisi mkoani hapa ikiwachunguza wenzao waliokuwa wakiwalinda watuhumiwa wawili wa mauaji waliotoroka mikononi mwao, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, ametangaza donge la shilingi milioni tano kwa mtu au watu watakaofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Samwel Joseph Mtinange (26) au kwa jina maarufu Samu na Mohammed Shaban Limu (35) ambao pamoja na wenzao wanne Daud Lezire Mkumba (40), Mathias Kurwa (34), Said Florian Nkwera (26) na Swalihina Yohana (36) wote wakazi wa Usa, wilayani Arumeru, wanadaiwa kumuua aliyekuwa Mwenyekiti wa Tawi la Chadema Usa, Msafiri

Johnson Mbwambo, Aprili 27 mwaka huu.

“Tunachunguza tukio zima la kutoroka kwa mahabusu hao, siwezi kusema polisi waliokuwa kwenye ulinzi kama wapo rumande au la, lakini tukio hilo linachunguzwa,” alisema wakati akizungumza na waandishi wa habari jana bila kutaja majina ya polisi waliokuwa wakifanya ulinzi huo.

Alieleza kuwa watuhumiwa hao walitoroka wakiwa wanatolewa mahabusu iliyopo mahakamani kupelekwa kwenye karandinga tayari kwa kurudishwa magereza.

Alisema katika tukio hilo askari polisi aliyekuwa amebeba bunduki alipigwa kikumbo na kuanguka.

Hata hivyo, Kamanda Sabas, alisema watuhumiwa hao hawakufanikiwa kutoroka na bunduki hiyo aina ya Sub Mashine Gun (SMG) ingawa habari zilisema baada ya kutoroka nayo waliitelekeza kwenye mto ulio jirani na mahakama hiyo.

Aliomba mtu yeyote atakayepata taarifa kuhusiana na watuhumiwa hao kutoa taarifa kwa polisi na kwamba zawadi ya Sh. milioni 2.5 itatolewa kwa kila mtuhumiwa atakayekamatwa.

No comments:

Post a Comment