Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, October 16, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Tanzania na Oman zina mahusiano ya Kidamu na kindugu ambayo ni maalum sana yanayopaswa kudumishwa, kuthaminiwa na kuenziwa kwa dhati.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemuambia Mfalme Qaboos Bin Said katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika katika nyumba ya kifalme ya Al -Alam mara baada ya kuwasili katika Taifa la Kifalme la Oman jana tarehe 15.Octoba, kuanza ziara ya kiserikali ya siku 4.
"Tanzania na Oman zina mashirikiano maalum kuliko nchi nyingine yeyote duniani kwa sababu ya undugu wa damu uliopo baina ya watanzania na wa Oman, hivyo hii ni ziara maalum sana katika nchi zetu." Rais amemuambia Mfalme.
Mfalme Qaboos amekubaliana na Rais Kikwete na kumueleza kuwa ni muhimu mahusiano haya yakadumishwa zaidi kwa njia ya uwekezaji katika nyanja mbalimbali, hasa katika Viwanda.
Rais Kikwete amepokelewa rasmi kwa kupigiwa mizinga 21 na kuandaliwa chakula maalum cha usiku ambapo Rais na ujumbe wake wamehudhuria.
Katika ujumbe wake Rais amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof Sospeter Muhongo, Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe. Dr. Abdallah Kigoda, Waziri wa Kazi, Ushirika na Uwezeshaji , Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri Fedha wa Tanzania Mhe. Janet Mbene.
Katika Ziara hii, Rais amefuatana na wafanyibiashara kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambapo leo tarehe 16 Octoba,2012 atakuwa na kikao na wafanyabiashara wa Tanzania na Oman na hatimaye kutia saini makubaliano ya kibiashara na kiuchumi baina ya nchi mbili hizi.
Mbali na kufanya mkutano na wafanyibiashara, leo Rais atatembelea makumbusho ya jeshi na jioni atakutana tena na Mfalme kwa ajili ya chakula binafsi cha usiku.
Mwisho.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Muscat - Oman.
16 Oktoba, 2012
Chat Conversation End

No comments:

Post a Comment