Wafanyabiashara katika eneo la sokoni wilayani Makete wamemuagiza
Mwenyekiti wa soko hilo Bw. Hosea Mpandila na viongozi wenzake kwenda kumuona
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo na kumwambia kuwa wanaomba awasamehe
kulipia ushuru wa biashara zao kwani wanaelekeza fedha zao katika ujenzi wa Choo
sokoni hapo
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika sokoni hapo,
wafanya biashara hao wamesema, kutokana na choo wanachokitumia hivi sasa kujaa,
wanalazimika kujenga choo kingine mara moja hivyo wanamuomba mkurugenzi
awasamehe kulipia ushuru mpaka wamalize kujenga choo hicho
Katika mkutano huo wafanyabiashara hao wameamua kuwa kila mmoja wao
alipie mchango wa tsh. 10,000/= kwa ajili ya ujenzi huo mchango unaotakiwa
ulipwe mara moja
Mmoja wa wafanyabiashara hao aliyejitambulisha kwa jina la Mia
amesema kutokana na ulazima wa kuchangishana fedha kwa ajili ya ujenzi wa choo
sokoni hapo, gharama ya shilingi 10,000/- ni kubwa hivyo wanamuomba Mkurugenzi
kuwasamehe ushuru wa sh. 1,500/- hadi hapo watakapomaliza ujenzi huo
Suala la kwenda kumuomba mkurugenzi awasamehe kulipia ushuru
lililimtia hofu mwenyekiti wa soko Bw. Hosea Mpandila ya kwenda kumuomba
mkurugenzi kwa madai kuwa huenda asikubali jambo lililowafanya wafanyabiashara
hao kumuagiza kuwa ni lazima aende
“Sisi ndio tumekutuma na lazima ukatekeleze maana wewe unafanya kazi
na sisi na tunapokuwa na kero zetu lazima uzifikishe kunakohusika, wewe
unachoogopa nini wakati tuliokutuma ni sisi?” alisema Mia
Katika kikao hicho wamechaguliwa wajumbe wanne kushiriki kwenye
kamati mbili ambazo ni kamati ya fedha na ya ujenzi ambapo zote zina wajumbe
wanne na zimeagizwa kuanza kazi mara moja
Kwa
muda mrefu sasa kumekuwa na mgogoro wa ujenzi wa vyoo ingawa choo cha soko hilo
kilikuwa kimejaa muda mrefu, na ujenzi wa vyoo hivyo huenda ukawa mkombozi wa
tatizo hilo
No comments:
Post a Comment