Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, October 3, 2012

Uhakiki wa Vitambulisho vya Taifa waanza Ilala, Temeke

Uhakika wa majina ya walioomba kupatiwa vitambuliso vya taifa umeanza jijini Dar es Salaam katika wilaya za Temeke na Ilala.

Mamlaka ya Taifa ya Utambuzi (Nida) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo waliendelea kufuatilia ripoti ya kuhakiki majina hayo kwa wale wasio na sifa za kupatiwa vitambulisho hivyo katika wilaya zote.

Afisa Habari wa Nida, Thomas William, alisema jana kuwa Wilaya ya Kinondoni ndiyo haijaanza uhakiki huo.

Alisema ripoti kamili ya vipingamizi mkoani humo itatolewa baada ya uhakiki kukamilika katika wilaya zote.

Uandikishaji majina ya vitambulisho hivyo ulianza Juni, mwaka huu, mkoani humo, huku mikoa mingine iki
subiri.

No comments:

Post a Comment