Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 5, 2012

UJERUMANI YAIPA TANZANIA SH.BILIONI 352

anzania na Ujerumani zimesaini makubaliano ya msaada kwa ajili ya ushirikiano wa maendeleo ambapo Ujerumani imetoa msaada wa miaka mitatu kwa Tanzania kuanzia mwaka huu wa fedha 2012/13 hadi 2014/15  wenye thamani ya Euro milioni 176 (Sh. bilioni 352).

Makubaliano hayo yalitiwa saini jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa Ujerumani nchini, Klaus-Peter Brandes, kwa niaba ya nchi yake na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa.

Brandes alisema Ujerumani itaendelea kufanya kazi na Tanzania ili kulifikia lengo la pamoja la kupambana na umaskini na kuboresha ubora wa huduma kwa wananchi na hasa wanaoishi vijijini.

“Leo tumesaini ahadi ya kihistoria.Kwa kipindi cha karibu miongo mitano iliyopita, ushirikiano wetu umeweza kutoa fedha zinazofikia karibu Euro bilioni 1.8. Na kwa fedha zilizotolewa leo, tumekubaliana ziende kwenye vipaumbele vya serikali, ambavyo ni maji, afya, maliasili na nishati,” alisema.

Dk. Mgimwa alisema fedha zilizotolewa zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili utekelezaji wa programu na miradi iliyoainishwa iweze kuchangia kwa kiwango kikubwa kwenye Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (Mkukuta).

“Kati ya fedha hizo, zitakazokwenda kwenye bajeti ni Euro milioni 18, programu za kuboresha menejimenti ya fedha za umma ni Euro milioni mbili, maji Euro milioni 45, afya Euro milioni 42.5, nishati Euro milioni 26,  maliasili Euro 31.5 na Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa  Euro milioni tatu na nusu,” alisema.

Maeneo mengine yatakayofaidika ni pamoja na serikali za mitaa Euro milioni 6.5 na Mfuko wa Masomo na Wataalamu Euro milioni moja.

No comments:

Post a Comment