Makovu
ya kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yamezidi kukitesa
chama hicho baada ya tathmini kuonyesha kuwa makundi yaliyotokana na
uchaguzi huo ndiyo yaliyosababisha kushindwa udiwani kwenye kata saba.
Katika uchaguzi uliofanyika katika kata
29, CCM kilishinda kata 22 na kupoteza kata saba ambazo zilikwenda kwa
vyama vya Chadema, TLP na CUF.
Akizungumza katika mkutano wa kuwashukuru
wananchi kwa kumchagua diwani wa CCM katika Kata ya Msalato, Katibu Mkuu
wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT), Amina Makilagi, alisema hayo
yalibainika katika kikao cha tathmini kilichofanywa na Sektarieti ya
Halmashauri Kuu mjini hapa juzi.
Makilagi ambaye pia ni Mbunge wa Viti
Maalum, alisema walibaini utaratibu wa kura za maoni ambao unataka
mshindi kuwa na zaidi ya nusu ya kura zote za wapiga kura ulisababisha
makundi.
“Siyo kwanza tulishindwa katika kata hizo
kwa sababu CCM haipendwi, bali tumebaini kuwa utaratibu ule wa kumpata
mshindi kwa zaidi ya nusu ya kura zote zinazopigwa unafaa kutumika
katika chaguzi za ndani ya chama,” alisema.
Alisema katika baadhi ya kata hizo baada
ya uchaguzi kurudiwa kwa mara ya pili, alipatikana mshindi mwingine na
hivyo kusababisha makundi.
“Haya makundi yalisema bora tukose wote ndio maana tukashindwa siyo kwamba wananchi walikuwa wakivitaka vyama hivyo,” alisema.
Matokeo ya uchaguzi huo wa Oktoba 27,
mwaka huu Chadema kilishinda katika kata tano na kukifanya kuongeza
madiwani watatu. TLP na CUF kila kimoja kilipata kata moja.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment