Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, November 9, 2012

David Kafulila amkera Pinda..!



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amemtaka Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, kuacha kumshinikiza kutoa kauli bungeni zinazoweza kushughulikiwa na halmashauri yake.
Alitoa kauli hiyo jana wakati wa kipindi cha maswali ya hapo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, baada ya Kafulila kuhoji utaratibu unaotumika wa kuwapa wawekezaji wa nje maeneo makubwa ya ardhi kuyamiliki huku wazawa wakikosa haki hiyo kama ilivyo katika mkoa wake.
Alimataka Waziri Mkuu kutoa kauli kwa kuwa Watanzania na nchi ya Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo ardhi ni alama ya ujamaa ambayo wanaweza kuishika kwa ajili ya kujikimu kimaisha.
“Utaratibu wa kuacha ardhi mikononi mwa mabeberu na wananchi kunyang’anywa na watu wanaojiita wawekezaji…tunataka Waziri Mkuu utoe kauli,” alisema Kafulila.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alisema serikali inazingatia maslahi ya wananchi wake na kwamba hakuna kitakachofanyika katika ugawaji wa ardhi bila halmashauri husika.
“Hili jambo kwanza mngelizungumza katika halmashauri ya Kasulu kabla ya kulileta hapa kama likishindika ndio muishauri serikali ili tufanyekaze kwa pamoja,” alisema.
Pinda alimshauri Kafulila akiwa sehemu ya baraza la madiwani kulishughulikia suala hilo kwenye halmashauri kwa kuwa liko ndani ya uwezo wa halmashauri yao.
“Kafulila amekiri kwamba jambo hilo limepita kwenye halmashauri yake. Mashinikizo yasiyo na msingi, mambo yamefanyika kwenye halmashauri yenu halafu unakuja kunikoromea hapa na kunishinikiza nitoe kauli nenda kaongee na halmashauri yako,” alisema Pinda huku akiokenaka kukerwa na shinikizo la mbunge huyo.
Hata hivyo, alisema kama kuna watu wanataka kuwekeza kwenye ardhi kwa ajili ya kuiendeleza, haoni kama ni dhambi na kutaka wawekezaji wasikatishwe tamaa.
Katika swali lake la nyongeza, Kafulila alimwambia Waziri Mkuu kuwa yeye anaona wawekezaji kupewa ardhi ni dhambi na kuhoji utaratibu uliotumika kutoa hekta 10,000 na ekari 25,000 za ardhi kwa mwekezaji wa Agroso na Felisa.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment