Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, November 13, 2012

MSANII WA MUZIKI WA TAARABU MARIAM KHAMIS WA TOT PLUS AFARIKI DUNIA ...!


Mariam Khamis enzi za uhai wake
 
Msanii nyota wa kundi la TOT plus taarabu nchini Mariam Khamis amefariki Mariam Khamis maarufu kama paka mapepe amefariki dunia alfajiri ya kuamkia leo mara baada ya kujifungua katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam .
Marehemu Mariam Khamis enzi za uhai wake amewahi kufanya kazi na makundi kadhaa yanayofanya mziki wa taarabu nchini ikiwemo East Africa Melody, Zanzibar Stars na 5 Stars. Baba wa marehemu Bwana Khamis Muhidini Shomary amesema mipango ya mazishi inaendelea kufanyika na marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho Magomeni Kota jijini Dar es Salaam

Chanzo: www.chingaone.blogspot.com

No comments:

Post a Comment