Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, November 9, 2012

Sumatra yazifungia daladala 14 Dar..!


Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Maji na Nchi kavu (Sumatra) imezifungia daladala14 kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.
Daladala hizo zimekamatwa na kufungiwa kwa mwezi mmoja katika oparesheni maalum iliyoanza juzi na inayoendeshwa na Sumatra kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kosa la kukatisha safari.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Afisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki wa Sumatra, Kondrad Shio, alisema oparesheni hiyo imeanzishwa kwa ajili ya kubaini na kudhibiti makosa yanayofanywa na baadhi ya madereva wanapokuwa barabarani yakiwamo ya kupandisha nauli pamoja na manyanyaso ya kubugudhi abiria.
“Hii oparesheni tumeianza na itakuwa ni endelevu kwa ajili ya kubaini yale makosa yanayofanywa na baadhi ya madereva hususani katika barabara zote kuu tano za hapa jijini na endapo gari ikimaliza muda huo wa mwezi mmoja tangu kufungiwa, basi tunahitaji mmiliki wagari hiyo amuajiri dereva mwingine,” alisema Shio.
Aliwataka abiria kutoa ushirikiano kwa Mamlaka hiyo na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa pindi wanapoona makosa hayo yanatendeka au yanatarajiwa kutendwa badala ya kuyanyamazia kwani madereva hao wanakiuka sheria za usafirishaji.
Shio alisema mpaka jana, kuna zaidi ya magari 30 yaliyokamatwa kwa makosa hayo hayo, hatua iliyomlazimisha kutoa namba za simu kwa wananchi kwa ajili ya kutoa taarifa pindi wanaposhuhudia makosa hayo.
Namba hizo ni 0767 250550, 0755 660016 na 0783 223013.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment