Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, November 9, 2012

Uamsho walalamikia hali ngumu gerezani..!


Viongozi wanane wa Jumuiya ya Uamsho, wametakiwa kufungua kesi ya madai kama wanahisi haki zao za kikatiba zimevunjwa wakiwa kizuizini katika Gereza la Kiinua Miguu, mjini Zanzibar.
Msimamo huo umetolewa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Ramadhan Nasib, baada ya upande wa utetezi kuwasilisha malalamiko kuwa wateja wao wamekuwa wakinyimwa huduma muhimu kama vile chakula cha nyumbani, kutojichanganya na mahabusu au wafungwa na badala yake kila mmoja kufungiwa katika selo yake.
Malalamiko mengine yaliyowasilishwa na Wakili Salum Tawfiq ni pamoja na kutopata uhuru wa kuabudu kwa kusali swala ya Ijumaa ya pamoja, kutobadilisha nguo zao, kufungiwa saa 24 bila ya kupata mwangaza wa jua na kunyimwa kusoma kitabu kitakatifu cha Qur’an.
Ramadhan Nassib kutoka ofisi ya Mwendesha Mashitaka Zanzibar akisaidiwa na Raya Mselem, aliileza mahakama kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 25 A(1) cha Katiba ya Zanzibar, mtu yeyote anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu, iwapo ataona katiba imevunjwa au haki zake zinaelekea kuvunjwa, Mahakama Kuu itakuwa na uwezo wa kumtaka afisa yeyote au chombo chochote cha serikali kutoa taarifa inayohitajika na mahakama kuu inaweza kufanya hivyo kwa kuombwa au kwa uamuzi wake yenyewe' kinaeleza kifungu hicho.
Raya Mselem alidai kesi hiyo ni ya jinai, na madai yake yanatakiwa kufuata mwenendo wa uendeshaji wa kesi za jinai, na kuiomba mahakama isiyatilie maanani maombi hayo badala yake malalamiko hayo yawasilishwe kunakohusika.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment