Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, February 23, 2013

BOJ COMPANY LTD YA MJINI MOSHI YADHAMINI FILAMU YA GHOST OF MY MOM

Kundi la CHOPER ART’S GROUP la mjini moshi ambalo kwa sasa lipo kambini katika kijiji cha Soko ndani ya kata ya Kahe katika wilaya ya Mwanga kwa ajili ya Maandalizi ya mwisho ya kufanya Filamu yao inayokwenda kwa Jina la GHOST OF MY MOM.
Kundi hilo ambalo limepata sapoti kubwa kutoka kwa kampuni ya DRM INVESTMENT chini ya mkurugenzi wake Rosemary Migire sasa Kundi hilo limepata Sapoti nyingine kutoka kwa kampuni ya BOJ COMPANY LTD ya mjini Moshi. 
 Baadhi yaWasanii wa Choper art's Group wakiwa katika pozi kabla ya kuanza safari ya kuelekea kambini.BOJ COMPANY LTD kampuni ambayo inajihusisha na usambazaji wa vifaa vya maofisini, Mashuleni, Vifaa vya Computer n.k iliyopo katika jengo la Vodacom mjini Moshi  Gorofa ya kwanza Room namba 117, Imejitolea kuhakikisha wanawasaidia vijana hao mpaka kukamilisha filamu hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kuchukuliwa picha ya video Tarehe nne mwezi wa Tatu chini ya Kampuni ya Uwezo video Production ya jijini Dar es Salaam chini ya Mtaalamu wa video Farid Uwezo, Huku ikiwa chini ya Muongozaji anayekuja kwa kasi katika kuongoza video Bora Lea Mwendamseke au maarufu kama Lamata.

No comments:

Post a Comment