Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, April 27, 2013

HAYA NDIO MAHAFALI YA SABA YA CHUO CHA GREEN BIRD WILAYANI MWANGA...!

 
Wahitimu wa chuo cha Green Bird wakiingia ukumbini.


Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Green Bird Education ndugu Juma H. Mndeme akitoa neno la shukrani.


Wanafunzi waliohitimu katika chuo cha Green Bird wakikabidhiwa vyeti.

LEO tarehe 27 April 2013 ni siku ya mahafali ya saba ya wahitimu wa kozi ya ualimu na kozi ya Biashara katika chuo cha Green Bird kilichopo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro. Chuo cha Green Bird ni chuo kilicho ndani ya taasisi ya Green Bird ambayo inajumuisha shule ya bweni ya Green Bird Girls na Green Bird Boys ambayo inatoa elimu ya kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita, pia ndani ya taasisi hii hii kunatolewa elimu ya awali ya kindergarten na elimu ya msingi. Katika chuo cha ualimu cha Green Bird kunatolewa kozi ya ualimu kwa daraja la cheti na diploma na pia kuna kozi ya biashara. Leo katika mahafali ya Wahitimu wa Kozi ya Ualimu na Biashara kulikuwa na wageni mbalimbali na Mgeni Rasmi alikua ni Afisa elimu wa Wilaya ya Mwanga Ndugu Mwenda.

Katika hotuba ya mgeni rasmi  ambaye ni afisa elimu wilaya ya Mwanga amewaomba wahitimu baada ya kufanya mitihani wafikirie kuomba vituo vya kazi katika wilaya ya Mwanga kwani wilaya ya Mwanga inawahitaji sana na pia ametoa shukrani kwa taasisi ya elimu ya Green Bird pamoja na Kalua Development Trust Fund kwa kuweza kushirikiana na jamii ya wilaya ya Mwanga kuhakikisha elimu inayotolewa na taasisi ya Elimu ya Green Bird inawanufaisha watu wa wilaya ya Mwanga pia alitumia fursa hiyo kuwaasa wazazi kuwapa watoto wao elimu huku akimwaga sifa kwa Green Bird kwa kiwango chao cha ada hasa kwa ngazi ya chuo ambacho ni kiwango cha chini kuliko vyuo vyote vya watu binafsi. Na elimu wanayotoa ni zaidi ya vyuo vingine.
 
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kalua Development Trust Fund Mama Mndeme alitumia fursa hii kuwaasa wahitimu wakawe mifano bora huko wanakwenda na elimu waliyopata ikawe manufaa kwa taifa. Pia mkuu wa chuo cha ualimu Green Bird Madame Saumu Khalifa katika hotuba yake ameeleza maendeleo ya chuo hicho pamoja na mipango ya baadae ikiwa lengo la chuo ni kuhakikisha kinakua chuo kikuu baada ya mwaka mmoja.

Huyu ndio aliyekua mshereheshaji wa maafali ya Green Bird anaefahamika kwa jina la Casim Mwinyi.(Babi)

No comments:

Post a Comment