Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, April 27, 2013

MUANDISHI AMERUDI....,

                                                  NYEMO CHILONGANI

Katika Maisha kila mtu anaweza, Fikra za kuwa upo peke yeke kwa kile anachokifanya pasipo kujua kuwa kuna watu wenye uwezo kama yeye na zaidi ya yeye katika kufanya jambo analofanya tatizo ni hajapata fursa ile uliyo nayo. Katika zunguka zunguka yangu jijini Dar es Salaam. Hapo ndipo nikajikuta nimetokea Tandale. 
Vijana waliokaa chini ya nuzo ya umeme ambayo juu yake wametundika bendera yenye jina la Kempu ya vijana wa eneo lile huku wakiwa kimya kumsikiliza kijana mmoja aliyeonekana ni muongeaji sana. Nilijisogeza na kutaka kusikiliza kama naweza pata chochote cha kuandika kulingana na kazi yangu. Nilijikuta nikivutiwa na hadithi alizokua anapiga yule kijana, Uhalisi wa hadithi ulinifanya kutaka kumjua zaidi. Baada ya kumaliza kisa kimoja cha Mwanamke wa ndoto nilijikuta nikimpa mkono na kumuomba tuongee pembeni.
"Naitwa Qassim Mwinyi niMuandishi wa habari sijui wewe unaitwa nani?"
"Naitwa Nyemo Chilongani"
Alijibu kwa uchangamfu nikagundua kitu kingine kwa kijana huyu ni jasiri na mwenye kujiamini sana.
"Ile hadithi umeitoa wapi?
"Ah natungaga mwenyewe"
"Eh kwani una hadithi ngapimpaka sasa"
"Nina hadithi zaidi ya Elfu mbilinimeziweka tu nyumbani"
"Dah ningependa kusoma moja ya hadithi zako"
"Ok usijali kwa kuwa wewe ni Muandishi nitakupa hadithi moja inaitwa Muandishi Amerudi"
"Kwanini umechagua kunipa hadithi hiyo niisome"
"We nenda kasome kisha ukiweza wape wasomaji wako wasome"
Alinipahadithi ikiwa katika cdnilienda nyumbani sikutaka kupumzika nikafungua kompyuta mpakato na kufungua hadithi ile.  Nilianza kusoma kwa shauku mpaka naimaliza nilijikuta nikilia zaidi ya mara nne. Nimeona nisiisome mwenyewe Anzia kesho hadithi hii itawajia Hapa.

No comments:

Post a Comment