Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, April 27, 2013

HUYU NDIO PRODUCER WA SauzWest Productions KATIKA HARAKATI ZA KUKUZA MUZIKI...!

Upande wa kulia ni MarkDen  akiwa na wasanii wa mkoani Kilimanjaro


MarkDen akifanya kazi katika studio ya SauzWest Productions

             MUZIKI wa Tanzania umezidi kufanya vizuri siku hadi siku na kuwapatia vijana wengi sana ajira ikiwepo kuwapa mafanikio makubwa kama kumiliki nyumba za kifahari na kuendesha magari mazuri na ya gharama. Lakini chakushangaza ni kwamba kwa mkoa wa Kilimanjaro imekua kama ni balaa kwa kuwa ndio mkoa mkongwe kwa upande wa kaskazini ambao haujapata mafanikio katika mziki wa kizazi kipya ukifananisha na mkoa kama Tanga na Arusha. Nilifanya juhudi za kuweza kumtafuta mmoja kati ya maproder ambao ni mkongwe sana kwenye fani ya kuandaa muziki. Nadhani wakazi wengi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro mtakua mnamfamu.

Jamaa huyo anaitwa  Mark Denning maarufu kama MarkDen anaishi Mabruda Street, Soweto Moshi na Najihusisha na Utayarishaji wa Muziki katika Studio za SauzWest Production. Na ana miaka kumi (10) kwenye utayarishaji wa muziki alianza kujifunza kutengeneza ala za muziki mwaka 2003 alipokua anasoma Chuo cha JRIIT (Aptech) na kuanza kazi studio ya Kwanza inayoitwa Nad Records mwaka 2007 hadi 2009 aliendelea kupractice bila kuwa na studio hadi alipofungua studio yake mwenyewe July 2012 inayofahamika kwa jina la SauzWest Productions.
 
Baada ya kufahamu hayo machache pia nilimuuliza ni vikwazo gani unavyokutana navyo kwenye kazi zako? "Vikwazo ni vingi kama unavyojua Mkoa wetu kwa tasnia hii ya burudani bado haijakua kwa kiwango kinachohitajika kwa hiyo kusikiza mbali inakua ngumu ila sasaivi naona wasanii baadhi wameamua kuwa serious na kazi zao kwa hiyo itafanya muziki wa Kilimanjaro upande kidogo, kikwazo kingine ni kipato kwani kama kipato kingekua kizuri tungekua tumeshafika mbali kwa kufanya kazi nzuri na kuzifanyia promosheni ya kutosha, Kikwazo kingine ni Tanesco ambao wamekua wakivuruga program za studio Pale huduma yao inapokuwa haipo na kuna ratiba studio Kwa kweli vikwazo vipo ila nimejipanga kupambana navyo." Alijibu MarkDen
 
Nilitaka watu wafahamu kwamba ni nyimbo gani ambayo umeitengeneza ambayo unahisi kama ndio imekufanya ukapata heshima kubwa sana kwenye shuhuli yako ya kuandaa muziki? "Nimefanya kazi nyingi nzuri…siwezi kusema moja ila kuna kazi kama Tupo Maficho niliifanya mwaka 2008 ndani ya Nad Records iliweza kunipaheshima kwenye media za huku kaskazini hasa A Town ila kwa sasa kuna kazi nimezitoa zinakubalika sana kwenye Radio za Moshi na bado tunaendelea kuzisambaza inaitwa Moshi_The Revolution Army pamoja na Shinikizo la Mawazo ambazo zote zimetoka SauzWest production na pamoja na kazi ya kutengeneza SOUNDTRACK ya Documentary ya KAULI NGO wa Marekani kwa hiyo kazi nyingi zipo nab bado tunajaribu kuangalia ipi ni Bora tuirelease." Alijibu MarkDen

Unadhani kati ya producer na msanii ni yupi anatakiwa kuheshimika endapo nyimbo itafanya vizuri? "Nadhani Producer ndio inabidi aheshimike japokua pia msanii nilazima nae apewe sifa zake kama amefanya kazi nzuri ila umaliziaji na utundu na akili ya Producer katika Mixing na Mastering ndio vinabidi kuheshimika zaidi kwa hiyo Producers inabidi waheshimike zaidi japokuwa nyimbo ikifanya vizuri msanii huwa ndio anafaidika zaidi." Alijibu MarkDen

Hapa mkoa wa Kilimanjaro unahisi kama wasanii, producers na watangazaji au maDJs mnaushirikiano mzuri kwenye kufanikisha harakati za muziki? 
"Swali Zuri kwa kweli kuna ushirikiano kidogo sana baina ya hao watu Umewataja inahitajika kuanzisha ushirikiano endelevu na wenye nia moja ya kupandisha muziki wetu juu na hii bila ushirikiano wa kutosha baina yetu inakua ni vigumu sana kufanikiwa….Hii ikiwa sawa basi harakati zetu zitaeleweka zaidi." Alijibu MarkDen

Unadhani nini kifanyike ili kuweza kuleta mafanikio ya muziki katika mkoa wa Kilimanjaro?

"Nadhani hii inaanzia kwa msanii ndio inaendelea kwamba wasanii wa Kilimanjaro
wajitahidi kuwa serious na kazi hii.Msanii akishakuwa vizuri inaelekea studio kwa producers kufanya kazi zenye viwango na baadae managers wawaandalie wasanii wao Video nzuri na baadae madj na watangazaji wa redio za nyumbani Kilimanjaro kuwasaidia wasanii nyimbo zao kusikika na kupata air time ya kutosha ndipo mapromoters wenye nia njema wajitokeze nakutengeneza matamasha ili kila mtu afaidi huu mziki wetu uliojificha. " Alijibu MarkDen

Wewe kama producer ni juhudi gani binafsi ambazo unazifanya kufanikisha mziki hususani wa wasanii wanaotokea Kilimanjaro? 
"Najitahidi sana kuwaelekeza wasanii ambao bado hawajatoka jinsi ya kujipanga kufanya kazi nzuri na pia kuwasadia wasanii kwa kuwatoza fedha kidogo ambayo inawezesha tu uendeshaji na ufanyaji wa kazi yake.Kwa sasa narekodi kwa kiasi kidogo sana cha fesha." Alijibu MarkDen

Wewe ni producer na pia unaimba, Kuna lawama kwamba nyie maproducers ambao mnaimba na mna studio huku mikoani huwa mnawarekodia wasanii wachanga kwenye studio zenu alafu nyie mnaenda kwenye studio kubwa zilizopo dar es salaam na kurekodi ngoma kwenye production nzuri? 
"Mimi pia ni msanii na nilianza kwanza kuwa msanii miaka ya 1998 na nikiwa na marehemu BT Boy na kundi letu la Dark Gz ila mnamo mwaka 2006 nilianzisha kundi la wasanii waimbaji na wanaorap ambao pia kwenye kundi hilo kuna maproducers wanne, Kundi la The Revolution Army linaloundwa na Mimi Mwenyewe MarkDen pamoja na
· Madi LegendinTown (Rapper/Writer)
· ST/STIM/Mfupa (Rapper/Writer)
· Sige Art (Paint artist/Rapper/Singer/Writer/Producer)
· Matata Deo (Singer/Rapper/Producer/Writer)
· Chie Nassa (Rapper/Singer/Writer/Producer)
· Nacz (Rapper/Writer/ )
Kwahiyo baada kuanza kuimba na kurap ndio nilipo anza kutayarisha muziki na tokea nimekua na studio sijawahi kurekodia Dar mara ya mwisho ilikua mwanzoni mwa mwaka 2007 niliporekodi track yangu pale Aiges Records nikimshirikisha Ngwea na Mez B kwa hiyo sio tabia yangu labda kwa maproducers wengine."
Alijibu MarkDen

Mtu akitaka kukupata kufanya kazi na wewe anaweza kukupaje? 
"Unaweza kunitafuta kwenye namba yangu ya mkononi ambayo ni 0717935546 ama ukaniandikia email kwenda mcdenning@gmail.com ama aje studio iliyopo Mabruda Street karibu na Makanyaga Pub Soweto Moshi.Pia unaweza kunipata facebook kwa Username Mark Denning na page la label ya studio kwenye https://www.facebook.com/SauzWestProduction na pia unaweza kusikiliza nyimbo nilizotayarisha kwa kupitia http://www.reverbnation.com/markden pamoja na http://www.hulkshare.com/SauzWest_Product na pia twitter kwa account ya #sauzwestproduct" Alijibu MarkDen


logo ya SauzWest Productions

No comments:

Post a Comment