Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, April 26, 2013

HAYA NDIO MAKOSA YALIYOMKOSESHA MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA DHAMANA...!

Mh. Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini kulia akiwa na vyombo vya sheria.

Hakika sikutaka kukurupuka kuposti kitu chochote leo kuhusu kadhia hii… kwanza sikuamini kama Jeshi letu pamoja na Mkuu wangu wa mkoa wa Arusha alikuwa na kesi ya kumfikisha Mbunge Kipenzi cha wana Arusha maakamani.

Lakini kubwa zaidi nilijuwa busara za Mkuu wetu huyo ambaye ni mtoto wa aliyekuwa msaidizi wa Katibu mkuu wizara ya utumishi (mama yake) japo angalikuwa na busara hata chembe kama mama yake, nakili wazi uwezo wake niliubeba zaidi ya uwasilia wake ulivyo.

Naomba niwasilishe kwanza mashtaka ya Kamanda mpambanaji G. Lema nikirudi nitajadili na kuwaletea maojiano ya mkuu wetu wa mkoa alivyo zungumza na Radi 5 leo pamoja na Video ambazo polisi walilazimika kufanya upekuzi wa masaa kadha kuzitafuta nyumbani kwa Lema.

Kwa mujibu wa wakili wa mbuge wa Arusha Mwanasheria Humphrey Mtui makosa aliyoshitakiwa nayo Lema ni haya:-1. Kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa (Worth fighting for). {HAPO KOSA NI UCHOCHEZI}

2. Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off. Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’ {HAPO KOSA NI UCHOCHEZI}

3. Kosa la Tatu ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’ {HAPO KOSA NI UCHOCHEZI}

Hayo ndiyo makosa mabayo yamemyima Mh. Lema  dhamana. hayo ndiyo makosa yaliyosababisha polisi watumie fedha za walipa kodi kumvamia usiku kurusha fataki badala ya kutumia busara ya kumuita tu kituoni na kusababisha taharuki maeneo hayo na ndani ya nyumba yenye ndugu jamaa na hata mtoto mwenye miezi mitano huku polisi wakitumia nguvu na kukiuka sheria

Huo umeitwa uchochezi baada ya mkuu wa mkoa kumtumia ujumbe wa mkononi kupitia simu yake kupitia namba 0752960276 aliyotishia kumbambikizia kesi anayoitaka yeye.

No comments:

Post a Comment