Taarifa zilizotufikia hivi punde ni
kwamba bomu limelipuka katika kanisa katoliki, parokia mpya ya
Olasiti iliyokuwa inazinduliwa leo jijini arusha. Bomu limelipuka wakati waumini wa kanisa la katoliki wakijiandaa na misa ya uzinduzi wa parokia hiyo.
Ambapo mpaka sasa haijajulikana idadi kamili ya watu waliojeruhiwa ama kupoteza maisha lakini taarifa za awali zinasema kuwa baadhi ya majeruhi wamekimbizwa hospitali.
Chanzo cha mlipuko huo inasemekana kuwa kuna gari ndogo ilifika kanisani hapo na kusimama. Baadae alishuka mtu aliyekuwa amevalia vazi mithili ya kanzu na kurusha kitu kuelekea kanisani ambacho ndicho kilichosababisha mlipuko huo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni balozi wa Vatican nchini Tanzania. Ambapo yupo baada ya kunusurika katika mlipuko huo wa bomu.
Timu nzima ya mtandao huu wa www.kingjofa.blogspot.com unawapa pole sana wamini wote wa kanisa la katolini na pia watu wote walioguswa na kitondo hicho cha kinyama.
Hizi ni taarifa za awali tu lakini kwa taarifa zaidi kuhusiana na mlipuko huo endelea kutembelea mtandao huu wa www.kingjofa.blogspot.com
No comments:
Post a Comment