Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, May 5, 2013

HIKI NDICHO WALICHOKISEMA MKUU WA MKOA WA ARUSHA, RPC NA Mh. LEMA BAADA YA KUFIKA KWENYE KANISA LILILOLIPULIWA KWA BOMU...!

Godbless Lema ambaye ni mbunge wa Arusha na ametembelea eneo la kanisa lililolipuliwa na bomu na kuwafariji wahanga wa tukio hilo. Akiongea kwa jazba na hasira na wananchi waliopo eneo la tukio, Lema ameitumu serikali kwa mara nyingine na kudai kuwa uzembe wa viongozi ndo chanzo cha matukio kama haya.

Hotuba fupi na nasaha zake zilikuwa zikisikika moja kwa moja kupitia Radio maria kabla ya kituo hicho kuamua kukatisha nasaha zake. Haijafahamika mara moja sababu za kukatishwa kwa hotuba yake.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo tayari amefika eneo ambalo ndio kanisa la katoliki lililolipuliwa na bomu lilipo na kuwafariji wahanga wa tukio la bomu.

RPC wa mkoa wa Arusha naye aliambatana na mkuu wa mkoa na muda huu alikuwa anatoa nasaha zake kwa wananchi. RPC ameeleza kuwa tukio hili ni la kigaidi. Katika maelezo yake, RPC amesema kuwa aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa kujificha na kurusha bomu.


Amesema Polisi wanawasaka waliohusika na unyama huu na ameomba yeyote mwenye taarifa yoyote aisaidie polis. Mpaka sasa watu waliojeruhiwa na bomu hilo ni 50 ambao wana majeraha ya kawaida ila kuna watu watatu hawa wapo mahututi.


Na mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi kuhusu mlipuko huo wa bomu.

No comments:

Post a Comment