Zikiwa zimesalia Takribani siku 34 ili kuweza kufikia katika Tamasha la kumi na sita la nchi za majahazi lijulikanalo kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF) kwa mwaka wa 2013 ambapo linategemewa kuanza mnamo Tarehe 29 ya mwezi wa sita mpaka Tarehe Saba ya Mwezi wa saba mwaka wa 2013.
Katika kuhakikisha ZIFF inanufaisha watengenezaji wa Film wa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
ZIFF sasa inapokea maombi kutoka kwa watengenezaji
filamu Afrika Mashariki wanaotaka kushiriki katika warsha ya utengenezaji
filamu wakati wa ZIFF mwaka huu..
Wanafunzi 5 (mmoja toka kila nchi ya Afrika Mashariki)
watalipiwa safari, malazi na chakula ili kushiriki kwenye warsha hiyo.
Wanafunzi 5 wengine watajilipia wenyewe.
Mfumo wa warsha utakuwa ni kufuatilia kikundi cha
watengeneza filamu walio tayari mafundi watakaokuwa wanatengeneza filamu fupi
wakati wa ZIFF. Utengenezaji huu unaitwa Guerilla Filmmaking (yaani filamu
chapchap) na katika siku 6 filamu itapigwa, itahaririwa na kuonyeshwa ZIFF siku
ya mwisho.
Wanaotaka kushiriki kwenye warsha watume maombi yao
hivi:
CV fupi.
Maelezo kwa nini wachaguliwe (maneno 1000)
Maombi yatumwe kwa: workshop@ziff.or.tz
Warsha
imedhaminiwa na Goethe
Institute na GIZ (Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani) na Jumuia ya
Africa Mashariki (EAC)
Maelezo
pia yako www.ziff.or.tz
No comments:
Post a Comment