Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, July 26, 2013

MWANAFUNZI WA KIKE AJIUA KWA SUMU BAADA YA KUBAKWA SUMBAWANGA...

Moja ya aina za sumu ya panya.
Mwanafunzi wa kidato cha nne, Flora Athanas (18) wa sekondari Mzindakaya wilayani hapa amejiua kwa sumu ya panya, baada ya kubakwa na mtu asiyefahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, alisema jana kuwa mwanafunzi huyo alibakwa usiku wa kuamkia Jumanne yeye na mwenzake, katika chumba walimopanga, kutokana na kukosekana kwa mabweni katika shule hiyo.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, siku hiyo Flora alikuwa na wanafunzi wenzake watatu, akiishi nao katika chumba hicho.
Inadaiwa usiku mtu asiyefahamika, alivamia nyumba walimopanga, akafunga vyumba vya wanafunzi wengine na kuingia chumba cha akina Flora akiwa na kisu na kuwatishia kuwa atakayepiga kelele atamuua kwa kisu.
Kutokana na tishio hilo, inadaiwa wanafunzi hao walikaa kimya na mvamizi huyo kumbaka Flora na mwenzake na kumwacha mwingine na kukimbilia kusikojulikana. 
Asubuhi siku hiyo, Flora aliamka, akatoroka na kwenda katika   duka kijijini hapo na kununua sumu ya panya.
Inadaiwa aliondoka na sumu hiyo kwenda porini nje kidogo ya kijiji cha Kaengesa, ambako hufanyika mnada wa hadhara na kukatisha maisha  yake kwa sumu hiyo.
“Uchunguzi wa awali wa Polisi unaonesha kuwa kifo hicho  kimesababishwa na hasira ya msichana huyo,“ alisema Kamanda Mwaruanda.
Aliongeza kuwa mwanafunzi mwenzake aliyebakwa pamoja naye, alifikishwa katika kituo cha afya Kaengesa, na kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu kuthibitisha kubakwa kwake.
Katika kituo hicho, ndiko pia mwili wa marehemu ulipelekwa kwa uchunguzi na kuthibitika kuwa chanzo cha kifo hicho ni sumu ya panya.

No comments:

Post a Comment