Mkuu
wa kitengo cha mawasiliano serikalini toka Wizara ya kazi na ajira
Ridhiwan Wema akieleza kwa waandishi wa habari juu ya mpango wa serikali
kupitia Wizara hiyo kukuza ajira kwa vijana wahitimu wa vyuo vya Elimu
ya Juu katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari leo
Jijini Dar Es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa.
Jijini Dar Es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa.
Na Hassan Silayo- Maelezo
Serikali
kupitia wizara ya Kazi na Ajira imepania kuondoa tatizo la ajira nchini
kwa vijana wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu, kwa kuanzisha mpango
maalum utakaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na vyuo vya elimu ya
juu nchini, Taasisi za fedha na wabia wa maendeleo.
Katika
mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Ridhiwan Wema, amesema
kutokana na tatizo la ajira nchini hasa kwa wahitimu vyuo vikuu,
Serikali kupitia Wizara ya Kazi na Ajira tumeamua kushirikiana na vyuo
vya elimu ya juu nchini, Taasisi za fedha na wabia wa maendeleo ili
kuweza kukabiliana na changamoto hii.
Katika
kuhakikisha serikali inatekeleza azma hii tayari Wizara imeanzisha
Idara ya kilimo, uchumi na Biashara katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoine (DAEA-SUA) na tayari Serikali imefanya makubaliano na Benki ya
CRDB kuanza utoaji wa mikopo kwa vijana mara utekelezaji wa mpango huu
utakapoanza.
Mpango
huu ambao utatekelezwa kwa awamu tatu utaweza kuwawezesha vijana 30,000
kupitia miradi 1,000 inayolengwa kuanzishwa katika awamu zote.
Aidha
Ridhiwani ameongeza kuwa uanzishwaji wa miradi hii unalenga
kuwanufaisha wengi kwani miradi hiyo itawezeshwa na kuzalisha ajira kwa
vijana wengine zaidi ya 26,000 na hii ikiwa ni lengo la serikali
kutimiza azma yake ya kuondoa tatizo la ajira kwa vijana nchini.
Ridiwani
ameongeza kuwa Jumla ya shilingi bilioni 54.451 zitahitajika kwa
kipindi cha miaka 3 ya utekelezaji wa program, ambapo shilingi Bilioni
50 zitawekwa dhamana na shilingi bilioni 4.451 zitatumika katika mafunzo
na kuwaandaa vijana ili waweze kukopesheka.
Utaratibu
wa ukopeshaji ni wastani wa shilingi milioni 50 hadi 300 kulingana na
mradi na Utaratibu wa utekelezaji na viwango vya riba, utaainishwa
katika mpango kazi wa utekelezaji program.
Source: MO Blog
No comments:
Post a Comment