Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, July 26, 2013

WACHIMBAJI WA TANZANITE WAOMBA UCHUNGUZI UFANYIKE KUHUSU TUKIO LA MWENZAO KUWAWA KWA RISASI

Baadhi ya wachimbaji wa mgodi wa Tanzanite katika Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara unaomilikiwa na Jackson Simon ambao ni miongoni mwa migodi minne iliyosimamishwa kufanya kazi kupisha uchunguzi wa kifo cha mchimbaji wa kampuni ya TanzaniteOne Willy Mushi wakizungumza na waandishi wa habari kuiomba Serikali kuifungulia migodi hiyo.

Chama cha wachimbaji madini wadogo wa Mkoa wa Manyara (MAREMA) Tawi la Mirerani Wilayani Simanjiro, wameiomba Serikali ifanyie uchunguzi kwa umakini na haraka, kifo cha mchimbaji aliyeuawa kwa kupigwa risasi ili migodi minne iliyosimamishwa iendelee kufanya kazi.
Mwenyekiti wa Marema Tawi la Mirerani, Japhari Matambi akizungumza na waandishi wa habari juzi alisema wanaiomba Serikali ichunguze kwa haraka suala hilo ili uchimbaji katika migodi hiyo minne uendelee.
Matambi alisema hawaishiniki Serikali ila wanaiomba ifanye uchunguzi wake kwa utaalamu na umahiri ili shughuli za uchimbaji kwenye migodi hiyo zirejee mara moja kwani jamii imeathirika kutokana na migodi hiyo kusimamishwa.
Alisema kutokana na Serikali kusitisha shughuli za uchimbaji kwenye migodi hiyo ya wachimbaji wadogo kitalu D, hadi uchunguzi wa kifo cha Willy Mushi mchimbaji wa kampuni ya TanzaniteOne utakapokamilika, watu 2,000 wamekosa ajira.
Alisema kutokana na Serikali kupitia Kamishana Msaidizi wa madini kanda ya kaskazini Benjamin Mchwampaka, kusimamisha uchimbaji kwenye migodi hiyo minne, wachimbaji 2,000 na familia zao wameathirika kwa kukosa kipato.
Katibu wa Marema, Tawi la Mirerani, Abubakari Madiwa akisoma tamko la chama hicho alisema wamesikitishwa na kifo cha mchimbaji wa kampuni ya TanzaniteOne kwani hakuna mtu yeyote anayefurahia mwenzake kuuawa.
Madiwa alisema wamesikitishwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kunukuliwa na vyombo vya habari wakimtuhumu mchimbaji mwenzao Joseph Mwakipesile (Chusa) kuwa amempiga risasi mfanyakazi wa kampuni ya TanzaniteOne.
“Hii ni sawa na kumhukumu kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanakosea yeye atabaki kuwa mtuhuhumiwa baada ya vyombo vilivyopewa mamlaka kuthibitisha kuwa amefanya kitendo hicho,” alisema Madiwa.
Alisema wamesikitishwa na kitendo cha wafanyakazi wa kampuni ya TanzaniteOne kutaka kuandamana kwa kutokuwa na imani na ofisi ya madini mkazi, ofisi ya madini kanda na askari polisi wa kituo cha Mirerani. 
“Kitendo cha kuhusishwa kwa Joseph Mwakipesile Chusa na viongozi wa ngazi za juu na kudai kuwa ameiweka Serikali mfukoni ni kitendo cha kuwachafua kwani hakuna mtu anayeweza kuiweka Serikali mfukoni,” alisema Madiwa.
Alisema wao kama viongozi wa chama cha wachimbaji madini wana imani na viongozi wa madini ofisi ya Mirerani, ofisi ya kanda na askari wa kituo cha polisi Mirerani na wanaomba wapewe ushirikiano kwani wanafanya kazi kwa umakini.
 
Chanzo: Woindeshizza Blog

No comments:

Post a Comment